TETEMEKO la ardhi lenye kipimo cha 5.7 limeikumba mikoa ya kanda ya ziwa hususan mkoa wa Kagera pembezoni mwa Ziwa Victoria leo Jumamosi Septemba 10, 2016.
Kwa mujibu wa taasisi ya Kimarekani ya U.S.G tetemeko hilo lilipiga urefu wa kwenda chini kilomita 10 na limeutikisa mji wa Bukoba na viunga vyake majira ya mchana.
Taarifa za awali kutoka mkoani humo zimesema, nyumba kadhaa zimebomoka.
Toa Maoni Yako:
0 comments: