Meneja wa Kituo cha kufua umeme kinyerezi I, Mhandisi Lucas Busunge, akifungua kikao cha ujirani mwema kati ya TANESCO, TPDC na viongozi wa jamii inayozunguka Vituo vya kufua umeme wa Gesi vya Kineterezi jijini Dar es Salaam Septemba 30, 2016.

Mkuu wa Kitengo cha Usalama, TANESCO Makao makuu, Misana Gamba
 
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said.

SHIRIKA la Umeme nchini TANESCO na viongozi wa dini, vyombo vya dola na viongozi wa Serikali za Mitaa sita inayozungu vituo vya kufua umeme wa Gesi asili vya Kinyerezi jijini Dar es Salaam, wamekubaliana kuweka mikakati ya pamoja kuhakikisha jamii inashiriki katika ulinzi wa miundombinu ya umeme.

Makubaliano hayo yamefikiwa leo Septemba 30, 2016, kwenye kikao cha ujirani mwema kati ya TANESCO, TPDC, viongozi wa dini, viongozi wa serikali za mitaa na vyombo vya dola ili kujadili namna bora ya kulinda miundombinu ya umeme kwenye vituo hivyo.

“Umeme wa Gesi ni umeme salama kabisa, hata hivyo ni wajibu wetu kushirikiana pamoja kuhakikisha miundombinu ya umeme huu wa Gesi inatunzwa na kulindwa,”, Meneja wa Kituo cha Umeme Kinyerezi I, Mhandisi Lucas Busunge alianza kwa kusema wakati akiwakaribisha wajumbe kwenye kikao hicho.

Tumeona tuitane hapa leo ili tujadiliane pamoja namna bora ya kuhakikisha umeme huu
utokanao na Gesi ambao Serikali imeiingia gharama kubwa, miundombinu yake
inalindwa na nyinyi viongozi mnao wajibu mkubwa wa kuwafikishia ujumbe wananchi
wanaoishi maeneo yanayozunguka mitambo hii. Alisema Mhandisi Busunge.

Akitoa mada juu ya Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa miundombinu ya umeme wa Gesi na hasara inayoweza kulikumba taifa na jamii kwa ujumla, Mkuu wa Usalama wa TANESCO makao makuu, Misana Gamba alisema, “Lazima tutambue kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa vituo hivi na fedha hizi ni za walipa kodi wa Tanzania, kwa hivyo ni wajibu wetu sote na sio TANESCO pekee kuhakikisha tunalinda miundombinu hii kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo,” alisema Gamba

Akifafanua zaidi, Mkuu huyo wa usalama alibainisha mambo ambayo jamii inapaswa kuelewa kuwa
ni hatari dhidi ya miundombinu ya umeme ambayo ni pamoja na kuwasha moto, kulima au kuchimba mchanga, mmomonyoko wa udongo, wezi wa vyuma, uvuvi haramu, kujenga, kufanya biashara au kuendesha magari makubwa sehemu ambayo miundombinu hiyo ya umeme wa Gesi inapita.

Mkuu huyo wa usalama wa TANESCO alisema, hatari inayoweza kutokea endapo mambo hayo
yatafanywa ni pamoja na kurudisha nyuma jiyihada za Serikali katika kuwaletea umeme wananchi, lakini pia hatari ya kulipuka kwa mitambo hiyo ambapo madhama makubwa yanaweza kuwakumba wananchi.

Akichangia kwenye mazungumzo hayo, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, ambaye ndiye alikuwa muendesha kikao, alisema, Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO, imekuwa ikitoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kutunza miundombinu ya umeme kwa faida ya Watanzania wote, na hatua ya kikao hicho ni mwendelezo wa utoaji elimu na kuwataka viongozi hao kuwa mabalozi katika maeneo yao, kwenye nyumba za ibada, ili kusudi wananchi wengi waelewe umuhimu wa kuunza miundombinu ya umeme ambayo kimsingi ni mali ya Watanzania wote.

Mhandisi Busunge

Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji (aliyesimama), akizungumzia umuhimu wa viongozi wa mitaa kushirikiana na TANESCO katika kuelimisha umma, kutunza miundombinu ya umeme.

Afisa Usalama wa TANESCO makao makuu, Fidelis Almasi, akielezea namna viongozi wanavyoweza kushiriki katika kuelimisha wananchi umuhimu wa kutunza miundombinu ya umeme na athari za zitokanazo na uharibifu wa miundombinu hiyo kwa jamii na serikali

Mkuu wa upelelezi, Kituo cha polisi Sitakishari-Ukonga, MrakibuMsaidizi wa Polisi, (ASP), Hassan Okello, akiwatoa hofu viongzoi hao kuhusu kutunza siri wanapotoa taarifa za wahalifu na uhalifu na kwamba yeye binafsi yuko tayari siku zote kuhakikisha usalama kwenye eneo hilo unazingatiwa

Afisa Usalama Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini, (TPDC), Eliasi Muganda, amesema, mabomba mawili ya gesi tayari yana gesi na yako umbali wa kina cha mita 2 kutoka uso wa ardji na hivyo hayahitaji mgandamizo kutoka juu kwani ni hatari yanaeza kupata nyufa na kuvujisha Gesi.


Afisa Elimu wa Kata ya Kinyerezi, Mwalimu Mercy Mtei, (kulia), yeye amesema, atawashirikisha walimu na wanafunzi kueneza ujumbe kwenye jamii

Sheikh Juma Swaleh wa Msikiti wa Othman Bin-Afan wa Kinyerezi

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kichangani, Niyukuli Leonard (kulia)

Mchungaji Jacob Msami, akizungumza.

Ustaadhi Ally akizungumza.

Mchungaji Ariel Mungereja wa Kanisa la EAGT, Kinyerezi.

Afisa Usalama wa Kituo cha Kinyerezi I, Furaha Munisi, akifafanua mambo mbalimbali ya kiusalama ambayo viongozi hao wanapaswa kuyachukua na kuwaelimisha wananchi

Picha ya pamoja baada ya kikao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: