Mkurugenzi wa Legal Services Facility, Scholastica Julu, akizungumza na wadau waliofika katika hafla ya miaka mitano ya LSf.
Wajumbe wa Bodi wa Legal Services Facility katika picha ya pamoja
Mwenyekiti wa bodi ya Lsf , Joaquine De Mello akiakabidhi hundi kwa mmoja wa wanufaika.
Mnufaika wa Ruzuku kutoka taasisi ya TEWOREC akinyoosha hundi yake juu yenye thamani ya shilingi bilioni moja.
Wanufaika wa Ruzuku wakiwa katika picha ya Pamoja na Wajumbe wa bodi.
Mkurugenzi  wa Legal Services Facility, Scholastica Julu, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa LSf.

Na Humphrey Shao, Dar es Salaam.

WITO umetolewa kwa wadau wa sheria kusaidia kupunguza mahabusu Magerezani kutokana na wingi wao ambao aikuwa lazima kuweka humo .

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la kisheria lisilo la kiserikali la Legal Services Facility (LSF),Joaquine De Mello, wakati wa Hafla ya miaka mitano ya shirika hilo na kukabidhi fedha kwa mashirika mapya ya wanaufaika.

“Nimeweza kuzunguka magereza yote nchini na kujionea namna gani wafungwa walivyojazana kwa wingi lakini robo tatu ya wafungwa waliopo humo ni mahabusu ambao awaja hukumiwa” alisema Jaji Joaquine De Mello.

Aliongeza kuwa imefika wakati wa wasaidizi wa kisheria kuanza kuwasaidia watu kwa ngazi ya vituo vya Polisi ambapo huko wanaweza kupata dhamana kabla ya kufika magarezani.

Kwa upande wake, Scholastica Julu, Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo alisema kuwa shirika hilo limeweza kutoa fedha zaidi ya Bilioni ishirini kwa mashirika mbalimbali na bado litaendelea kutoa hili kuweza kusaidia wasaidzi wa kisheria na Mashirika yanayowasimamia .

Alisema kuwa wameweza kupokea changamoto ya usafiri kwenye baadhi ya mikoa na kama shirika wanalifanyia kazi hilo swala hili waweze kutatua tatizo hilo kwa wasaidizi wanaofanya kazi hiyo kwa mazingira hayo magumu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: