Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea msaada wa fedha kiasi cha dola laki mbili (USD 200,000) kutoka kwa Balozi wa Uganda hapa nchini Doroth Samali Hyuha wapili kutoka (kushoto) akiwa pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uganda Elibariki Maleko. Msaada huo umetolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kuwasaidia wahanga wa Tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi mchango wa fedha kiasi cha dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) uliotolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Uganda hapa nchini Doroth Samali Hyuha mara baada ya kuwasilisha mchango wa kiasi cha fedha Dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni. PICHA NA IKULU.
Toa Maoni Yako:
0 comments: