Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupewa dhamana.
mwenyekiti wa UVCCM akiwa anatoka mahakamani mara baada yakupewa dhamana
Na Woinde Shizza, Arusha.
Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imemsomea mashtaka mawili Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Lengai Ole Sabaya ambaye pia ni diwani wa kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha vijijini.
Miongoni mwa makosa hayo aliyosomewa mahakamani hapo kosa la kwanza alituhumiwa kujifanya Afisa mtumishi wa serikali (TISS) huku kosa la pili ikiwa kugushi moja ya nyaraka za serikali (kitambulisho).
Akisoma mashtaka hayo mahakamani hapo Wakili wa serikali, Lilian Mmasi alisema kuwa Mnamo
May 18 katika hotel ya Sky way iliopo makao mapya jijini Arusha Mshitakiwa alijitambulisha kama Afisa utumishi wa idara ya usalama wa taifa na kufanya Utapeli.
Wakili Mmasi alitaja kosa la pili ambalo Mshitakiwa Lengai Ole Sabaya alisomewa kuwa
ni kugushi kitambulisho cha idara ya usalama wa Taifa kilichokuwa kikisomeka Jamuhuri ya muungano wa Tanzania idara ya usalama wa Taifa (TISS) Lengai Ole Sabaya kikosi maalumu
Agent (undercover) chenye code no MT 86117 huku akitambua kuwa ni kinyume cha kisheria.
Hata hivyo mara baada ya kusomewa mashtaka hayo mahakamani hapo mtuhumiwa alikana mashtaka ndipo Hakimu Mkazi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Gwantwa Mwamkuga
Alisema dhamana ipo wazi iwapo wathamini watakidhi vigezo vinavyotakiwa na
mahakama hiyo.
Hata hivyo Mshitakiwa alipata dhamana baada ya kukidhi vigezo vilivyowekwa na
mahakama ambapo ilikuwa ni wadhamini wawili wenye sifa ambapo kwanza awe mtumishi wa serikali pili awe na mali isiyohamishika yenye thamani ya shilingi milioni tatu kwa kila mmoja.
Kesi imeahirishwa na hakimu mkazi hadi itapotajwa tena Oktoba 5 ambapo uchunguzi unatarajiwa kukamilika na kesi hiyo kuanza kusikilizwa.
Mara baada yakupata dhamana mahakamani hapo wakili wa mtuhumiwa, Yoyo Asubui alisema kuwa mshtakiwa amesomewa mashtaka yote mawili na kukana mashtaka ambapo wanatarajia uchunguzi
ukikamilika kesi itaanza kusikilizwa mapema na haki kutendeka huku akimtaka mteja wake kuendelea na majukumu ya mandeleo kwa wananchi wa kata ya Sambasha.
“Kwakweli kesi hii sio ya kweli na naweza kusema ipo kisiasa na nashukuru Jeshi la Polisi kwa kunishikilia na kukaa na mimi vyema hadi kunileta mahakamani ambapo naamini haki itatendeka na ukweli utabainika “Alisema Sabaya mara baada ya kupata dhamana
Alisema kuwa hili limetokea mara baada ya kuwatoa wabadhilifu wa mali za umoja wa vijana (UVCCM) ambapo kwa muda mrefu wamekuwa mali za umoja huo kujinufaisha wenyewe na vijana kukosa maendeleo kupitia miradi ya umoja huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: