Timu ya Morogoro wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la uchampioni wa Airtel Rising Stars 2016 kwa upande wa wavulana. Morogoro iliifunga Ilala 1-0 katika fainali iliyopigwa kwenye uwanja wa Karume, Dar es Salaam jana.
Temeke wasichana wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe la uchampioni wa Airtel Rising Stars 2016. Temeke waliishinda Ilala 5-4 katika changamoto ya mikwaju ya penati.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye akimkabidhi nahodha wa Temeke wasichana Shamimu Hamisi kombe la ubigwa wa Airtel Rising Stars 2016. Temeke waliishinda Ilala 5-4 katika changamoto ya mikwaju ya penati.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania wakimkabidhi nahodha wa Temeke wasichana Shamimu Hamisi kombe la ubigwa wa Airtel Rising Stars 2016. Temeke waliishinda Ilala 5-4 katika changamoto ya mikwaju ya penati.
---
Goli pekee lililofungwa na mshambuliaji hatari Tepesi Evans wa Morogoro lilitosha kuifanya timu hiyo kuwa mabingwa wa michuano ya vijana chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars 2016 kwa kuwafunga Ilala 1-0. Mechi hiyo ambayo ilikuwa ya kuvutiwa yenye upinzani mkali ilishuhudiwa na mamia ya mashabiki akiwepo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye.
Baada ya kosa kosa nyingi, Evans aliachia shuti kali mnamo dakika 77 ya mchezo, shuti ambalo lilienda moja kwa moja na kuamsha shangwe na nderemo kutoka kwa mashabiki. Juhudi za Ilala kuzawashisha hazikuzaa matunda mpaka mchezo unamalizika.
Mchezo huo ulikuwa ni kama marudio ya mechi ya Alhamisi ambapo timu hizo zilikutana kwenye hatua ya makundi huku Ilala ikitoka kichwa chini kwa kukubali kichapo cha 2-0.
Akifunga michuano hiyo ya kila mwaka, Waziri Nnauye alisema kuwa serikali inaunga mkono juhudi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na wadhamini. ‘Kwa kuwapa fursa wasichana na wavulana hawa kuonyesha vipaji vyao, ni kusaidia kubadilisha maisha yao kwani mpira wa soka ni zaidi ya burundani – ni kufahamiana, kupata uzoefu na zaidi, ni ajira’, alisema Nnauye.
Naye Mkurungenzi Mtendaji Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema kampuni yake inajivunia mafanikio ya Airtel Rising Stars yaliyopatikana miaka tano iliyopita. ‘Wachezaji ambao waliisaidia Uganda kufuzu kwenye michuano ya AFCON 2017 Gabon ni uzao wa Airtel Rising Stars na ni uhakika hayo yatatokea Tanzania hivi karibuni’. Alisema Colaso huku akiongeza kuwa Airtel mpaka sasa ishawekeza Tshs2.4 billioni kwenye michuano hiyo.
Kwa upande wake Raisi wa TFF Jamal Malinzi alielezea michuano ya Airtel Rising Stars kama michuano ya kutumainiwa katika kuibua vipaji. ‘Serengeti Boys na timu ya Taifa ya Wanawake ni ushuhuda tosha wa mafainikio ya michuano hii’, alisema Malinzi.
Timu bora, wachezaji bora, waamuzi pamoja na makocha walipewa tuzo wakati wa fainali za michuano hiyo.
Timu ya Temeke wasichana walishinda ubingwa wa michuano hiyo kwa penati 5-4 baada ya kwenda sare ya 2-2 kwenye muda wa kawaida.
Wakati huo huo, timu ya Temeke wavulana walishinda nafasi ya tatu ya michuano hiyo kwa changamoto ya mikwaju ya penati ya 5-4 dhidi ya Kinondoni baada ya kutoka sare ya 0-0 kwenye muda wa kawaida.
Kinondoni wasichana walipata nafasi ya mshindi wa tatu baada ya kuwafunga wenzao Arusha 2-0. Magoli yote ya Kinondoni yalifungwa na Veronica Mapunda.
Toa Maoni Yako:
0 comments: