Tundu Lissu: baada nilishalala lakini maandishi hayaozi. Nimekusoma.
Those are simply usual innuendos from a usual and expected you. You did not address any of my major arguments. As usual, ukaishia kutukana na kutoa hogwash allegations kwamba tulipewa hela na CCM ili tugawe kura za ukawa. Sounds familiar evil-intentioned allegation. Unachosahau ni kwamba nyie haohao mliimba miezi mingi kwamba tulipewa hela na Lowassa ili tuanzishe Chama chake na kwamba angegombea kwenye Chama hicho. Alipowafuata mkanywea na kumeza fedheha. Wewe ni mwanasiasa uliyebarikiwa kutokuwa na mshipa wa aibu. Unabahati pia upo katika Jamii ambayo political morals ni kama hazipo. Ndiyo maana akina Chenge hadi leo wanaendelea kutamba.
Kuhusu uimara au udhaifu wa CUF. Utafanikiwa kuwadanganya wana CUF wajinga tu kwamba kura na wabunge waliopata ni kazi ya miezi miwili baada ya Lipumba kuondoka na malaika Lowassa kuingia ukawa.
CUF werevu hutawapata na wapo wengi na Ndiyo maana wenzako wanafanyia vikao Vuga. CUF werevu wanajua kwamba walifanya kazi miaka mitano kuvuna walichokivuna. CUF werevu wanajua mlituma watu wenu wachukue fomu hata Katika majimbo mliyokubaliana kuachiana. CUF werevu wanajua kwamba mlimwambia Anatropia kamwe asitoe jina lake huku Segerea na ndiyo maana mkamzawadia ubunge wa Viti maalumu. Endeleeni kuwadanganya CUF wajinga lakini CUF werevu wapo tele!
---
*ANAANDIKA TUNDU LISSU*
Profesa Kitila Mkumbo ana-imply kwamba CUF ya Profesa Lipumba na nje ya UKAWA itakuwa chama imara.
Kwa sababu anajua ni hoja uchwara isiyokuwa na msingi wowote katika hali halisi, Profesa Kitila Mkumbo anaongeza a rider kwamba haya ni maoni yake tu, sio lazima yawe ni 'facts.' Kwa nini msomi huyu anayesifika anatoa maoni without any basis in facts??? Ni usomi gani huu???
Profesa Kitila Mkumbo sio mjinga kiasi hicho, ni msomi na mtu mwerevu. Anajua what the facts are lakini hataki kuzisema kwa sababu they are inconvenient facts.
What are these inconvenient facts? ?? Ni hizi hapa: CUF ya Profesa Lipumba ilikuwa haiendi popote politically. Kilele cha CUF ya Lipumba ilikuwa Uchaguzi Mkuu wa '05 alipopata kura milioni 1.8. Baada ya hapo it's all downhill, by '10 Profesa Lipumba alipata kura laki 6, a whopping 66% drop.
Kwenye ubunge, CUF ya Profesa Lipumba ilikuwa haijawahi kupata wabunge zaidi ya wawili Bara. Which is to say, CUF iliyokuwa inamfichia Lipumba ni CUF ya Zanzibar ambayo haijawahi kushindwa uchaguzi Zanzibar tangu '95.
Ni ujambazi wa maCCM tu ndio ambao umewanyima CUF ya Zanzibar ushindi miaka yote hii. Kwa mara ya kwanza, kwa sababu ya kushirikiana na CHADEMA, CUF ya Tanganyika ilipata viti kumi vya ubunge Tanganyika.
Hii ni idadi kubwa ya wabunge wa kuchaguliwa kuliko wote wa '95, '00, '05 na '10 combined. Ya Zanzibar yanafahamika. These are indisputable facts, sio maoni. CUF ya Lipumba itakuwa na nguvu kuliko hizi zilizotokana na UKAWA? ??
Ni mjinga tu anayeweza kusema au kufikiria hivyo. Ni ujinga huo huo walio nao hao wanaomtumia Lipumba wakifikiria kwamba ataua UKAWA na CUF Zanzibar.
Kama uchaguzi wa mwaka jana is any guide, Profesa Lipumba akigombea hatakuwa tofauti na mgombea wa ACT ambaye licha mahela yote ya maCCM ili agawe kura za UKAWA, hakufikisha hata laki moja. Kwenye ubunge hatapata hata mmoja mmoja au wawili ambao alikuwa anawapata miaka ya nyuma.
Lipumba amebakia politically a walking corpse, bila mapolisi na usalama wa taifa na maCCM hawezi kuhutubu mkutano wa kitongoji.
He's finished. Hata mumpambe namna gani he's politically a dead man walking.
Anachokifanya hakitatuumiza in any meaningful way, hasa hasa kinatuondolea utando wa buibui kwenye fikra za wengi kwamba bado kuna upinzani nje ya UKAWA. Hakuna.
Toa Maoni Yako:
0 comments: