Na MatukiodaimaBlog

WANANCHI wilayani Mufindi mkoani Iringa wametakiwa kuanza maandalizi ya kunufaika na milioni 50 kwa kila kijiji zilizopangwa kutolewa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuanza kujiunga vikundi vya ujasiriamali na kuvisajili.

Wito huo umetolewa na mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa kutoka wilaya ya Mufindi, Marcelina Mkini (Pichani) wakati akizungumza na wanahabari kuhusu utaratibu huo mzuri ulioahidiwa na Rais Dkt. Magufuli wakati wa kampeni.

Alisema kuwa ili wananchi kuweza kunufaika na utaratibu huo ni lazima kujiunga katika vikundi vya watu wenye malengo yanayofanana na kuvisajili ili pindi pesa hizo zitakapotolewa kuweza kuzipata.

Mkini alisema kwa utaratibu wa fedha hizo hazitatolewa kwa mtu mmoja mmoja hivyo kwa wale ambao wanazitamani fedha hizo ni lazima kuanza kujiunga katika vikundi ambavyo vimesajiliwa.

"Lengo la Rais wetu ni kuona wananchi wananufaika na matunda ya nchi hii ndio sababu ya kuahidi kusaidia vijiji fedha hizo shilingi milioni 50 kwa kila kijiji fedha ambazo ni nyingi sana na zitasaidia wananchi kujikwamua katika dimbwi la umasikini ... lazima tumpongeze sana kwa mtazamo huu ambao haujapata kutokea"

Hivyo alitaka vijana, wanawake na wazee kujiunga makundi yenye malengo yanayofafa yakiwemo ya ufugaji kwa wazee ama kilimo na makundi mengine ambayo yatapelekea vijiji kuwa na vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) zao.

Mkini ambae pia ni mwenyekiti wa umoja wa wanawake Tanzania (CWT) wilaya hiyo ya Mufindi aliwataka viongozi wote wa UWT ngazi zote kusaidia kuhamasisha wanawake kuonyesha mfano katika kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali .

Huku akiwataka kwa kipindi hiki cha kuelekea kupata fedha hizo kuwa makini na matapeli ambao baadhi ya mikoa wameanza kujipitisha kudanganya wananchi kuwa fedha hizo zitapitia katika NGOs zaO.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: