Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi habari juu ya hatua ya serikali waliochukua kwa wanafunzi waliondolewa katika chuo kikuu cha Dodoma leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Kulia ni Naibu Katibu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo, Kulia ni Kamishina wa Elimu wa Wizara hiyo, Eustella Balamsesa.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

BAADA ya Serikali kufanya uchambuzi wa sifa za Wanafunzi wanaostahili kusoma program maalum ya Ualimu wa sekondari kwa masomo ya sayansi katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),ni wanafunzi 382 ndio wamekidhi kusoma program hiyo kati ya wanafunzi 7,805 waliondolewa katika mgomo wa walimu wa chuo hicho.

Akizungumza na waandishi habari Ofisini kwake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa wamefanya uchambuzi huo ili kutoa haki kwa watu wenye sifa ya kusoma program maalum kwa walimu wa sekondari.

Amesema kuwa vigezo vya wanafunzi hao kusoma ilikuwa ni ufaulu wa masomo ya sayansi kwa daraja C-A ambapo ni wanafunzi 382 ndio wameonekana na sifa hizo kati ya wanafunzi 6595 waliodahiliwa stashahada maalumu ya walimu wa sekondari .

Amesema wanafunzi 52 walipata daraja la nne katika matokeo ya kidato cha sita ambapo ni kinyume cha matakwa stashahada maalumu ya walimu wa sekondari .Amesema kuwa wanafunzi 1,210 walidahiliwa kimakosa kutokana kundi hilo ni walimu wa shule ya msingi ambao hawako katika program maalumu ya walimu wa sayansi.

Profesa Ndalichako amesema kuwa wanafunzi 4,586 wa mwaka wa kwanza program maalum ya stashahada ya walimu wa sekondari wamekidhi vigezo vya ufaulu lakini sio kwa masomo ya sayansi watahamishiwa katika vyuo vya serikali vya ualimu ambavyo ni ,Morogoro ,Butimba, Mpwapwa, Songea, pamoja na Tukuyu kuendelea na masomo yao huku wanafunzi wa 1,337 wa mwaka pili wanahamishiwa katika vyuo vya ualimu wa shule ya msingi ambavyo ni Korogwe na Kasulu na watajighramia na huku wanafunzi 290 hawana sifa kabisa ya kusoma na wizara kuwataka waombe mafunzo ya sifa zinazolingana.

Amesema wanafunzi 29 watahamishiwa kusoma mafunzo ya ualimu wa shule ya msingi katika chuo cha Kasulu kwa gharama zao huku 1181 wametakiwa kuomba mafunzo ya ualimu wa shule ya msingi katika chuo chochote kwa gharama zao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: