Meneja wa Bia ya Ndovu Red Malt, Nicholous John (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masoko TBL Kushila Thomas pamoja na Meneja Masoko wa vinywaji wa kampuni ya TBL Vimal Vaghmaria (wa kwanza kulia) wakionyesha kinywaji cha Ndovu Red Malt mara baada ya kuzindua kinywaji hicho jana katika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam ambapo wateja zaidi ya 50 walihudhuria katika hafla ya uzinduzi wake. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Meneja wa Bia ya Ndovu Red Malt, Nicholous John akiongea wakati wa Uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt uliofanyika jana katika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam ambapo wateja zaidi ya 50 walihudhuria katika hafla ya uzinduzi wake.
Meneja Masoko wa vinywaji wa kampuni ya TBL Vimal Vaghmaria amesema: “Ubunifu wa kila bidhaa yetu unalenga kukidhi matakwa ya watumiaji wake ambao ni wateja wetu ambao wanahitaji kutumia bia zilizo bora na zinazokwenda na wakati katika soko”.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Damian Soul akitoa burudani katika uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt uliofanyika jana katika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam.
Mkurugenzi wa Masoko TBL, Kushila Thomas (wa kwanza kushoto) akijadiliana jambo na Meneja wa Bia ya Ndovu Red Malt, Nicholous John (katikati) pamoja na mgeni mwaliko aliyefika katika uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt uliofanyika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam.
Wageni waalikwa wakijipatia bia ya Ndovu Red Malt.
Wageni waaalikwa wakibadilisha nawazo huku wakijipatia kinywaji cha Ndovu Red Malt.
Wageni waliohudhuria uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt uliofanyika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam.
Kinywaji cha Ndovu Red Malt.
Meneja wa Bia ya Ndovu Red Malt, Nicholous John (kushoto) akiwa na Msanii wa Kuchora Picha Bwana Lute (katikati) wakionyesha furaha yao mara baada ya uzinduzi wa bia hiyo.
Maua yaliyohudumia tukio hilo.
---
Katika mkakati wake wa kuendelea kuwaletea wateja wake bidhaa zenye bora wa hali ya juu, kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) imezindua bia mpya inayojulikana kama Ndovu Red Malt, bia ambayo imetengenezwa kwa kimea kwa asilimia 100 na ikiwa ni mwendelezo wa ubunifu wenye ubora wa bia ya Ndovu Special Malt inayoongoza kwa ubora na bia pendwa kwa watumiaji wengi wa bia nchini.
Bia ya Ndovu Red Malt imegundulika na kutengenezwa hapa nchini Tanzania ili kukidhi ladha ya wanywaji wa bia ikiwa na ubora wa kiwango cha juu na yenye ladha ya pekee kwa kulinganisha na aina nyinginezo za bia zilizopo kwenye soko.
Uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt umefanyika katika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini Dar e Salaam Julai 20 mwaka huu ambapo wateja zaidi ya 50 walihudhuria katika hafla ya uzinduzi wake.
Mbali na kuwa na ladha ya aina yake inayoleta burudani kwa watumiaji wake kutokana na kutengenezwa kwa Shahiri kwa asilimia kubwa pia bia ya Ndovu Red Malt inavutia kwa mwonekano wake wa rangi kuwa na rangi ya uwekundu kwa mbali.
Meneja Masoko wa vinywaji wa kampuni ya TBL Vimal Vaghmaria amesema: “Ubunifu wa kila bidhaa yetu unalenga kukidhi matakwa ya watumiaji wake ambao ni wateja wetu ambao wanahitaji kutumia bia zilizo bora na zinazokwenda na wakati katika soko”.
Alisema utengenezwaji wa bia ya Ndovu Red Malt kwa kutumia Shahiri kwa asilimia asilimia100 kunaleta upekee wa bia hii kwa kulinganisha na bia zingine kwenye soko na ina ladha tamu na mwonekano wake wa kuvutia ambao unaiongezea thamani.
Kwa upande wake, Mpishi Mkuu wa Bia wa Kiwanda cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Cavin Nkya, alisema kuwa bia hii mpya ya Ndovu Red Malt inazinduliwa ikiwa ni uthibitisho wa uwezo wa kampuni katika kuwapatia watanzania kinywaji chenye kiwango cha kimataifa na chenye ubora wa hali ya juu.
“Ndovu Red Malt ni bia ya daraja la kwanza inayodhihirisha dhamira yetu ya kuwapatia wateja kinywaji ambacho daima wametamani kukipata kikiwa kimesheheni radha murua nay a kipekee,” alisema Nkya.
Nkya alimalizia kwa kusema kwamba matokeo mazuri katika utayarishaji kinywaji hiki ni kutokana na uchanganyaji mahiri na wa umakini wa nafaka bora zinazozalisha hapa nchini ambazo zinazotumika kutengeneza bia Ndovu Red Malt.
Bia hii ina kiasi cha kilevi cha asilimia asilimia 4 na inapatikana katika chupa zenye muundo maridhawa zenye ujazo wa mililita 375 ,kama zilivyo aina nyingi za bia zinazozalishwa na kampuni ya TBL zilizopo sokoni.
Sasa, bia ya Ndovu Red Malt itaanza kupatikana sehemu zote nchini ambako kampuni inasambaza bidhaa zake kuanzia wiki hii kwa gharama ya shilingi 2,000/ kwa bei ya reja reja.
Toa Maoni Yako:
0 comments: