Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akiwasili katika Eneo la Ghana tayari kwa ukaguzi wa barabara inayopanuliwa na kujengwa kwa lami kwa kiwango cha Km 2.7.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella, akitoa maelekezo kwa Mtaalaam mshauri, namna gani wafanye ili kuweza kuepusha athari ya mafuriko pindi mvua zitakapo nyesha.
Moja ya Mainjinia wa Nyanza Roads works, alipokutwa kazini, wakati wa ziara ya Mhe, John Mongella Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kwenye ukaguzi wa barabara hiyo.
Mhandisi wa Maji mjini Mwanza, Mhandisi Sanga, akitoa maelezo kwa waandishi wa habari namna walivyo tekeleza, maazimio yakuhamisha miundo mbinu ya maji ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo ya makongoro.(Picha zote na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa).
Mhe. John Mongella Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akiongea na waandishi wa habari mara baada yakufanya ziara ya kukagua barabara ya Makongoro Uwanja wa Ndege inayopanuliwa na Mkandarasi Nyanza Road ya Jijini Mwanza na kutoa maelekezo yakuikabidhi barabara hiyo ifikapo Novemba, 2016.
---
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongella, ametembela na kujionea upanuzi wa wa barabara ya Uwanja wa Ndege Mwanza na kisha kuwawataka wananchi kuwa tayari kutoa ushirikiano kwa Serikali pindi inapohitaji kufanya shughuli za maendeleo.
Akiwa katika Eneo la Upanuzi wa barabara hiyo eneo la Ghana, amewapongeza wananchi wote waliotoa ushirikiano katika awamu ya kwanza kwakukubali kuondosha shughuli zao ambazo zilikuwa pembezoni mwa hifadhi ya barabara ili kupisha upanuzi unaofanyika hivi sasa wa Km. 2.7 kuanzia eneo la Ghana hadi Pasiansi
Katika hatua Nyingine Mongella amemuagiza Mkandarasi kuhakikisha anamaliza kazi hiyo kwa wakati ili kuondosha msongamano wa magari ambao umekuwa ni kero kwa wananchi hasa nyakati za asubuhi na jioni, Aidha Mongella, ameahidi kufanya ziara kila baada ya wiki mbili ili kujionea maendeleo ya barabara hiyo na kusema ifikapo Novemba 26 mwaka huu Mkandarasi awe amekabidhi kazi hiyo.
Upanuzi wa barabara hiyo Unafatia maamuzi yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli, kwa kuagiza kiasi cha fedha Bil.2.7 zilizokuwa zimetengwa kwaajili ya Sherehe za Muungano kubadilishiwa matumizi na kupelekwa kwenye upanuzi wa barabara hiyo ili kuondoa adha ya msongamano wa magari kwa wananchi husan ni wale wanao tumia barabara ya Uwanja wa Ndege.
Imetolewa na
Atley J. Kuni
Afisa Habari na Uhusiano- RS
Mwanza
13. Julai, 2016

Toa Maoni Yako:
0 comments: