Jana usiku niliingia mkoani Arusha. Baada ya juzi kula kiapo cha Maadili Ikulu Dar na leo pia kula kiapo cha Utii kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Komredi Daudi Ntibenda.

Baadae leo nimewasili katika wilaya yangu ya Longido na kuanza kazi kwa kufanya kikao cha kwanza na kundi muhimu katika ujenzi wa Longido yetu.

Nitumie fursa hii kuwaomba maoni na ushauri wenu kuhusu changamoto za Wilaya ya Longido.

Kwa hakika nipo tayari kushirikiana na viongozi wote bila kujali itikadi za vyama kwenye kusukuma maendeleo.

Karibu Longido.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: