Waombolezaji miongoni mwao wakiwemo waandishi wa habari wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa MpigaPicha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaamm akitokea nchini India ambako alipatwa na mauti.
Baadhi ya waombolezaji wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Senga wakiwa Uwanja wa Ndege wakisubiri wa mpendwa wao.
Maofisa wa Kampuni ya Kupakia na Kupakua Mizigo Uwanja wa Ndege, Swisport wakiutoa nje jeneza lenye mwili wa marehemu Joseph Senga.
Waombolezaji wakiuweka mwili wa marehemu Senga kwenye gari tayari kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Muhimbili.
Wanachama wa Press Photographers Tanzania wakishiriki kuingiza kwenye gari jeneza la mwili wa wa aliyekuwa mpiga picha za habari Tanzania, marehemu Senga.
Dada wa marehemu Joseph Senga, Yunista Senga akilia kwa uchungu alipoona jeneza lenye mwili wa kakake, Joseph Senga.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akielezea kwa masikitiko kuhusu msiba wa Joseph Senga.
Baadhi ya waombolezaji wakiwemo wapigapicha za habari wakiondoka Uwanja wa Ndege baada ya kuupokea mwili wa aliyekuwa mpiga picha mwenzao.
Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu tayari kwa safari ya kutoka uwanjani hapo kuelekea hospitali ya Muhimbili kuhifadhiwa. Marehemu Senga alifariki katikati
ya wiki hii nchini India, alikokwenda kwa matibabu. Taarifa za ndugu wa
marehemu kuhusu taratibu za mazishi zinasema, Mwili wa marehemu
umehifadhiwa kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili, ambapo kesho Jumapili
asubuhi utapelekwa nyumbani kwake Sinza, kwa ajili ya ibada fupi na
kisha utapelekwa viwanja vya Sinza-Uzuri kwa wananchi ndugu jamaa na
marafiki kuuuaga. Taarifa hiyo pia inasema, Mwili wa Marehemu
utasafirishwa kwenda Kwimba mkoani Mwanza kwa mazishi... baada ya zoezi la kuuaga Jumapili Julai 31, 2016. (PICHA
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said na RICHARD MWAIKENDA; KAMANDA WA MATUKIO BLOG.
Othman Michuzi (kulia) wa Blog ya Mtaa kwa Mtaa, akimfariji mpiga picha wa Tanzania Daima, Loveness Bernard ambaye alifanya kazi ofisi moja na marehemu Senga
Baadhi ya wapiga picha na waombolezaji wengine wakiondoka baada ya mwili kuwasili.
Gari lililobeba jeneza lenye mwili wa marehemu Senga, likiwa tayari kuondoka uwanjani hapo
Msafara wa magari ukiwa tayari kuondoka.
Toa Maoni Yako:
0 comments: