Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Ambapo alizungumzia juu ya biashara haramu ya binadamu ambayo imekuwa ikiendendeshwa na mtandao wa watu wasiowaaminifu kwa kuwalaghai mabinti wa Kitanzania kwa kuwaahidi kuwapa ajira nje ya nchi. Kwenye mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Watumishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kwa makini mkutano na waandishi wa habari.
Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakisikiliza na kunukuu yaliyokuwa yanazungumzwa na Mkuu wa kitengo Bi. Mindi Kasiga (hayupo pichani).
Mkutano na waandishi wa Habari ukiendelea.
---
Kumekuwa na matatizo mengi ambayo wamekuwa wakiyapata Watanzani wengi wanaokwenda nchi za nje kufanya kazi kwa minajiri ya kujipatia kipato, wengi wa watanzania hao ni Wasichana hasa wenye umri wa kati ya miaka 18 na 24 na hata chini ya umri huo.
Kufuatia
hali hiyo alitoa wito kwa Watanzania wote wawe makini na kujiridhisha na
mikataba ya ajira inayotambuliwa na Mamlaka za nchi unayotaka kwenda,
kwa hapa nyumbani mamlaka zinazoweza kukusaidia ni pamoja na Ofisi za
Ubalozi za nchi husika,Wakala wa Ajira Tanzania(TESA) kwa Tanzania Bara
au Kamisheni ya Kazi - Zanzibar.
---
Kumekuwa na matatizo mengi ambayo wamekuwa wakiyapata Watanzani wengi wanaokwenda nchi za nje kufanya kazi kwa minajiri ya kujipatia kipato, wengi wa watanzania hao ni Wasichana hasa wenye umri wa kati ya miaka 18 na 24 na hata chini ya umri huo.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na
Kimataifa, Mindi Kisiga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Bi Mindi Kisiga aliendelea kusema kuwa kwa miezi ya hivi karibuni hususani kati ya mwezi Machi-Mei 2016, Balozi
za Tanzania nchini Malaysia na India zimepokea maombi ya kusaidia
kuwarejesha nyumbani Watanzania ambao walipelekwa nchini India na
Thailand kwa ahadi za kupatiwa ajira.
Aliongeza kuwa ahadi hizo za ajira zimekuwa zikitolewa na watu wasio waaminifu ambao wanashukiwa kujihusisha na mtandao wa biashara ya kusafirisha binadamu 'human trafficking', mtandao ambao unahusisha raia wa Tanzaniana waliopo ndani na nje ya nchi kwa kushirikiana na raia wa kigeni waliopo kwenye nchi hizo.

Nchini
India pekee kuna Watanzania wapatao 500 walioripotiwa kuwa huko wakiwa
350 New Delhi, 45 Bangalore, Mumbai 20 na wengine wanaelekea Goa.
Watanzania hao hulazimishwa kuingia katika biashara ya
ukahaba, hunyang'anywa pasi za kusafiria na kulazimishwa kufanya shughuli
zingine tofauti na zile walizoahidiwa kabla ya kwenda huko.

Toa Maoni Yako:
0 comments: