Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza jambo wakati akiagana na Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa
Upako’ katika kanisa lake la Maombezi lililopo Ubungo Kibangu jijini
Dar es Salaam. Rais Dkt. Magufuli alihudhuria ibada hiyo pamoja na
kukagua barabara inayotoka Ubungo Kibangu hadi Barabara ya Mandela eneo
la Riverside.
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi Mchungaji Anthony Lusekelo ‘mzee wa
upako akiagana na mke wa Rais Mama Janeth Magufuli mara baada ya
kuhudhuria ibada katika Kanisa la Maombezi Ubungo Kibangu jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Rais Dkt. Magufuli akiwashukuru waumini (hawapo
pichani ) wa kanisa hilo la Maombezi la Mzee wa Upako.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli wakati wakitoka kwenye kanisa la Maombezi la Mchungaji Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU





Toa Maoni Yako:
0 comments: