Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na matukio ya kihalifu ya kuchoma moto nyumba, mashamba na kuharibu mazao yaliyotokea mkoa wa Kusini Pemba na kuahidi kuyashughulikia. Kulia ni Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omary Makame.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdani Omary Makame, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na matukio ya kihalifu ya kuchoma moto nyumba, mashamba na kuharibu mazao yaliyotokea mkoa wa Kusini Pemba. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Mkutano huo umefanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.
Makamanda wa Jeshi la Polisi na waandishi wa habari wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni katika mkutano kuhusiana na matukio ya kihalifu ya kuchoma moto nyumba, mashamba na kuharibu mazao yaliyotokea mkoa wa Kusini Pemba. (Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi). 
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI- WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: