Wakati mwingine haijalishi umeanzaje safari yako lakini..."Jinsi Utakavyoimaliza".
Kuna watu walianzaga vizuri na kumaliza vizuri "Hongera zao!"
Lakini wengine walianza vizuri, wakapotea njiani but hawakukata tamaa...walijikung'uta mavumbi na kuendelea mbele wakamaliza vizuri.
Kuna wengine walianza vizuri...wakafika njiani wakakata tamaa ya kuendelea, wakaishia pabaya.
Lakini ninachotaka kusema ni kwamba.....Kuanza jambo flan ni kitu rahisi sana, lakini tatizo lipo kwenye kumaliza (UNAMALIZAJE?).
Halafu the Funny Thing ni kwamba... Hakuna jambo lenye mwanzo lisilokuwa na mwisho! Wote sisi tunaishi mfumo flan wa maisha kwa sababu tuna matarajio flan ambayo ni mazuri kwetu. Mtume Paulo kwenye Kitabu Cha Matendo ya Mitume 20: 24 anasema, "Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu KAMA KUMALIZA MWENDO WANGU na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari Njema ya Neema ya Mungu"... Kwahiyo tunaona Uthamani Upo kwenye Kumaliza siyo Kuanza jambo. Pia kwenye 2Timothy 4: 6-8, Mtume Paulo anasema... "Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile...... "Kwahiyo... Kumbe Ukimaliza jambo vizuri,na kuvumilia mpaka mwisho; mwishoni kuna REWARD/TUZO pamoja na KURIDHIKA!
Hakuna Jambo Jema Kama Kumaliza Kile Ulichokianza!
Hakuna Jambo Jema Kama Kuona Ndoto au Maono Uliyokuwa nayo Muda Mrefu Yametmimia!
Hakuna Jambo Jema Kama Kuona Jambo Ulilolisugulia goti, Ukalivujia jasho muda mrefu likitokea mwishoni.
NI FURAHA YA AJABU MNO!!!
Nami nawaombea Kwa JINA LA YESU, Huyu MUNGU aliyewapa Neema ya Kuanza/Kuanzisha jambo au Kuwa na maono kuhusu jambo flani na awape Neema ya Kumaliza na Kuliona Likitokea na Kukamilika! Amen...
Toa Maoni Yako:
0 comments: