Mwanamuziki nguli wa
nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars,
Keri Hilson akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulifanyika
lagos nchini Nigeria
Mwanamuziki nguli wa
nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music Stars,
Keri Hilson akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulifanyika
lagos nchini Nigeria. Akishuhudia ni Mkurugenzi wa Masoko Airtel
Afrika, Dia Ezzaoudi.
Mshindi wa Airtel
Trace Music Stars Afrika 2015, Nalimi Mayunga akiongea wakati wa mkutano
na waandishi wa habari uliofanyika Lagos nchini Nigeria.
Mwanamuziki
nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music
Stars, Keri Hilson akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza
mkutano na waandishi wa habari
Mwanamuziki
nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel Trace Music
Stars, Keri Hilson akiwa katika picha pamoja na Mshindi wa Airtel Trace
Music Stars Afrika 2015, Nalimi Mayunga
Wafanyakazi
wa Airtel kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika picha pamoja na
Mwanamuziki nguli wa nchini Marekani na jaji mkuu wa shindano la Airtel
Trace Music Stars, Keri Hilson mara baada ya kumaliza mkutano na
waandishi wa habari. Pichani (wa pili kushoto) Afisa uhusiano wa Airtel
Tanzania, Bi Jane Matinde.
---
Mwanamuziki nguli nchini Marekani, Keri Hilson ameingia nchini Nigeria ili kushiriki katika shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika linaloshiriksha nchi 9 barani Afrika ambapo Tanzania inawakilishwa na mwanadada Melisa John.
Keri Hilson atashirikiana pamoja na majaji wengine katika kumtafuta mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika kwa mwaka 2016. Ambapo Taji la ushindi wa Airtel Trace Music Stars 2015 linashikiriwa na Nalimi Mayunga kutoka Tanzania
Siku moja baada ya kuwasili , Keri Hilson ameshiriki katika mkutano na waandishi wa habari ambapo alihainisha kuvutiwa kwake na washiriki na kukiri kwamba bara la Afrika lina vipaji vingi vya muziki na kuwapongeza Airtel na Trace kwa kuanzisha mpango huu wenye lengo la kuinua vipaji na kuwawezesha vijana kuvifikia ndoto zao
“Naamini finali itakuwa na mvuto sana nimekutana na washiriki na kushuhudia vipaji vya kutosha. Mambo makuu tutakayoangali wakati wa fainali ni pamoja na uwezo wa mshiriki kuweza kutoa burdani , uwezo wa sauti yake na jinsi gani anaweza kutoa burdani kwa mashabiki. Naamini mashindano ya kesho yatakuwa na mvuto nanimejiandaa vyema kufanya kazi na mshiriki atakayeshinda kwa mwaka huu”








Toa Maoni Yako:
0 comments: