Nyota wa filamu za Action nchini Tanzania ambaye ni mmoja kati ya mwasisi wa filamu hizo, Jimmy Mponda maarufu kama “J.Plus” aliyeanza rasimi kutoa Action Muvi ya “Shamba kubwa” mnamo mwaka 1994, Filamu yake ya pili ikafuata 1995, ilipewa jina la “Unga Adui” yatatu iliitwa “Kifo haramu” ilikuwa 1997 ya nne ilikuwa “Usia” 2003.

2005-2010 Jplus na Seba walienea kwenye masikio ya watu baada ya kutoa filamu ya “Misukosuko” iliyo dumu kwa muda wa miaka 5 bila kupoteza ubora wake kwenye masikio ya mashabiki. 2012 Jplus alitoa filamu ya “Double. J” ambayo tunaweza kusema ilikuwa kama filam yake ya mwisho kwa maana ya kwamba toka kipindi hicho J.plus hajatoa filamu yeyote mpaka hii leo.
​​
Refere: 2005 ilipotoka filamu ya “Misukosuko” kulikuwa na mgawanyiko wa mashakiki yaani kama team za mpira, Mashabiki wa “J.Plus” na Mashabiki wa Sebastian Mwanangulo maarufu kama “Inspector Seba” kutokana na mpambano wao katika muvi hiyo, Baada ya Part 1 na Part 2 kuisha Scene za “Seba” hazikuwepo tena ingawa Misukosuko iliendelea na Part zingine.

Hali hiyo ilipelekea wadau mbalimbali wa filamu kudhani kuwa wawili hao huenda wakawa labda waliingia kwenye mgogoro, lakini hakukua majibu ya uhakika yaliyo bainika kama kweli J.Plus na Seba walitofautiana kauli.
​ ​
Baada ya Kimya cha miaka 3 iliyopita nyota wa filamu hizo za Action “J.Plus” kupitia ‘Mzimuni Theatre Arts’ anategemea kuvunja ukimya 2016 kwa kuja upya na filamu mpya ya ‘The Foundation’ ( Msingi) ambayo kwa upande wake J.plus amesema “Nategemea hii filamu ya ‘The Foundation’ irudishe heshima ya Muvi za Action Tanzania kama ilivyo kuwa awali.

Hivyo wadau wangu na fans wang ambao walikuwa wanatamani kuona J.Plus na Seba wakicheza Filamu moja basi huu ni ujio mpya wenye kasi kubwa ‘The Foundation’ imechezwa na Jimmy Mponda a.k.a J.Plus, Sebastian Mwanangulo a.k.a Inspector Seba, Christina Aidan, Saidi Ndomboroa, Mariamu Mustafa, OP Mohamed a.ka Guga, Ramadhani Mohamed a.k.a Junior nk. Hivyo Staytuned, mtaarifu na mwenzio naomba mapokezi mema kutoka kwenu watanzania thanks.”
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: