Basi hilo likiwa limeteketea lote kwa moto mchana huu.
Basi la abiria mali ya Kampuni ya Tahmeed, lililokuwa likitokea Jijini Tanga kuelekea Jijini Dar es salaam, likiteketea kwa moto mchana huu katika eneo la Komkonga. Inaelezwa kuwa Ajali hiyo imetokea wakati Basi hilo likiwa limesimama baada ya Abiria mmoja kuomba msaada tutani "WA KENDA KUCHIMBA DAWA" ambapo baadhi ya Abiria wengine nao walishuka na kusikia harufu ya tairi linaloungua. muda mchache tu tairi hilo lilipasuka na moto kuanza kusambaa hadi kwenye tanki la Mafuta. Hakuna mtu yeyote aliepoteza Maisha kwenye ajali hii na hakuna mali iliyoweza kuokolewa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: