NGUVU ITUMIKAYO KUKAMATA WAHUJUMU UCHUMI WA SUKARI, endapo kama ingetumika kupambana na majangiri na waharamia wa wanyama pori, basi kwa hakika tungeweza kuokoa zaidi ya Tembo 90,000 waliouawa katika kipindi kimoja tu cha awamu ya serikali ya 4, kwa ajili ya biashara haramu ya pembe za ndovu!

Kwa sasa kg1 ya pembe za ndovu inathaminishwa kuwa ni TSh 4.5 Mill. na ikiwa kama pembe 1 ya ndovu inawastani wa kg30 basi itagharimu takribani Millioni 135 za Tz, ambapo fedha hiyo ni sawasawa na tani 750 za sukari iliyofichwa, na pia kama ni pembe zote 2 za tembo mmoja aliyeuawa basi itakuwa sawa na tani 1,500 za sukari, inayoweza kubebwa kwenye malori 50 yenye kontena kubwa za futi 40 kwa kila lori moja.

Mpaka hapo hoja yangu ni kwamba, katika kipindi cha miaka 10 iliyopita Tanzania tulipoteza zaidi ya Tembo 90,000 ambapo kwa wastani wa kila saa moja inakadiriwa kuwa Tembo mmoja aliuawa na maharamia hao haramu!! Kwa takwimu hizi, binafsi naona hii ni zaidi ya wahujumu sukari, ambapo kukamatwa na tani 4,500 za sukari ni sawa na Tembo watatu tu kati ya hao Tembo 90 elfu waliouawa katika kipindi cha miaka 10 iliyopita!

Mdau,
Emmanuel Seni - Mtwara.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: