Assalaam Aleikhum,
Updates za familia ya Ankal Issa Michuzi iliyopatwa na msiba wa kuondokewa na Mtoto wa Ankal, Maggid Muhidin (18), aliyefariki Jumapili Mei 8, 2016 huko Durban, Afrika Kusini:
Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa Mei 13, 2016 majira ya saa saba mchana kwa ndege ya shirika la Emirates kupitia Dubai (kwa kukosekana kwa ndege za moja kwa moja kuja nchini kutoka Durban). Mwili wa kijana wetu utapokelewa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere eneo la Cargo la Swissport, Jijini Dar es salaam.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi saa 10 alasiri katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. Taratibu za kuandaa mazishi zitaanza saa 4 asubuhi siku hiyo hiyo ya Jumamosi, nyumbani kwa mama wa marehemu kota za Wazo Hill, Tegeta, ulipo msiba.
NAMNA YA KUFIKA MSIBANI
Ukitokea Tegeta Kibaoni kama unaelekea Kiwanda cha Cement cha Wazo Hill, mbele mkono wako wa kulia kuna Kanisa la KKKT na ukienda mbele tena kidogo, utaona Bar yenye uzio wa rangi ya njano ambao umeandikwa "Twiga Cement", hapo pana bango linaloelekeza njia karibu na kituo cha Bajaji nje. Unaingia upande huo wa kulia mita 250 mbele unakata tena kulia, mita 70 mbele utakuta maturubai, ndipo msibani.
Innalillah wa inna ilayhi raajiun
-AMIN.



Toa Maoni Yako:
0 comments: