Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula akifungua rasmi mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye makao makuu ya shirika hilo Upanga jijini Dar es salaam ambapo alilipongeza shirika hilo kwa kazi nzuri ambayo wafanyakazi wake wanaifanya kwani ndiyo shirika pekee la Serikali linaloendeshwa kwa ufanisi mkubwa na kuiletea heshima serikali, Waziri Mabula amewaambia wafanyakazi wa shirika hilo pamoja na Menejimenti yake kuendelea na kazi nzuri ambayo wamekuwa wakiifanya ili kuleta maendeleo zaidi nchini katika sekta ya nyumba. PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM
Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu akizunguma na wafanyakazi wa shirika hilo kabla ya Waziri Angelina Mabula kuufungua rasmi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Nyumba wakifuatilia mkutano huo.
Wafanyakazi wa shirika la Nyumba wakiimba wimbo wa wafanyakazi kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo.
Wafanyakazi wa shirika la Nyumba wakiwa katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu na Naibu Waziri Angelina Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo baada ya kuufungua rasmi mkutano huo.
Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu na Naibu Waziri Angelina Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo baada ya kuufungua rasmi mkutano huo.

Toa Maoni Yako:
0 comments: