Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkaribisha Mke wa Waziri Mkuu
Mama Marry Majaliwa Ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam. Mama
Majaliwa alifika Ofisini hapo ili kujionea shughuli mbalimbali
zinazofanywa na mke wa Rais.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa akisaini kitabu cha wageni mara
baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli
Magogoni jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimuonesha Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa mafuta maalumu yanayotumiwa watu wenye ulemavu wa ngozi Albino ambayo atayagawa hivi karibuni kwa baadhi walemavu wa ngozi katika maeneo mbalimbali nchini. Pia Mke wa Rais mama Janeth amewaomba watanzania kuwajali Wazee na watu wenye ulemavu wa ngozi. PICHA NA IKULU.





Toa Maoni Yako:
0 comments: