JUZI Jumamosi, nimeona kitu hiki kwa mara ya pili, leo ningependa tujadili hapa kwa uwazi, bila ya matusi wala uoga.

Siku hizi kuna utaratibu wa kufanya usafi kila Jumamosi, NAUKUBALI. Lakini sasa naanza kuona kama unakwenda kwa mwendo wa uburuzaji na unataka kuleta uzembe... Watu hawatakiwi kufungua maduka hadi saa 5 asubuhi... atakayefanya hivyo anakamatwa na kutozwa faini ya Sh 50, 000.

Lakini ilivyo, watu humaliza shughuli za usafi hadi saa 3 asubuhi. Sasa zile saa mbili zilizobaki, vipi watu wasianze kutafuta riziki yao? Au kama ni uataratibu wa usafi, kila mtu inajulikana eneo analotakiwa kufanya, wakijumuika na kumaliza mapema, halafu waendelee kulala wakisubiri saa 5?

NAFIKIRI HII si SAWA NA VIONGOZI WANAPASWA KUTAFAKARI MAMBO MENGINE, SI KUFANYA TU... vizuri pia tukawa huru kueleza hoja tunazoamini ni sahihi. Waoga hawawezi kujenga taifa bora... katika hili ninaamini kuna walakini...

Na Mdau,

Saleh Ally.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: