
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanania Dk. Gharib Bilal (wa tatu kutoka kushotona) Mama Salma Kikwete (kwanza kushoto) wakishiriki mazishi ya marehemu Benadette Izengo mama wa Mkurugenzi wa kampuni ya Montage Limited, Teddy Mapunda aliyekaa katikati yao pamoja na wanafamilia wengine wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam mara baada ya ibada iliyofanyika kwenye kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph.

Mke wa Rais Mstaafu Dk Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete akiweka mchanga kaburini wakati aliposhiriki mazishi ya Marehemu Mama Benadette Izengo yaliyofanyika jana kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Balozi Asha Rose Migiro akiweka mchanga kaburini wakati wa maishi ya marehemu mama Benadette Izengo.
Padre Matumaini akiongoza ibada ya mazishi ya Marehemu Mama Benadette Izengo iliyofanyika kwenye kanisa la Mtakatifu Joseph jana.
Wanafamilia wakiwa katika ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye kanisa la Mtakatifu Joseph jana jijini Dar es salaam na kufuatiwa na mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni.
Teddy Mapunda na Ndugu yake wakiwa pembeni mwa jeneza la mama yao mpendwa marehemu Benadette Izengo.
Mkwe wa Marehemu mama Benadette Izengo akishiriki ibada ya mazishi pamoja na ndugu na jamaa wa familia kwenye kanisa la Mtakatifu Joseph jana.
Wajukuu wa marehemu wakishiriki ibada hiyo jana.
Wana familia wakiwa na majonzi kwa kuondokewa na mpendwa mama yao Marehemu Mama Benadette Izengo.
Mwenyekiti wa Chama cha UDP, Mzee John Cheyo akishiriki sakramenti ya bwana kutoka kwa Padre Kaombwe wakati wa ibada hiyo ya mazishi.
Teddy Mapunda na Mumewe Nestor Mapunda wakiwa na majonzi huku wakiangalia jeneza la mama yao mpendwa marehemu mama Benadette Izengo.
Baadhi ya waombolezaji wakishiriki mazishi kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
Kutoka kushoto ni Joseph Kusaga Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Entertainment, Nandi Mwiyombela, Justin Pamba, Godfrey Kusaga na John Mbele nao walishiriki katika mazishi hayo ya mama Bebadette Izengo.


Toa Maoni Yako:
0 comments: