Tukio wa wizi wa mifugo limeripotiwa kutokea wilayani Makambako. Kilichovuta hisia, ni mbinu waliyotumia wezi hao kumsafirisha ng'ombe aliyeibiwa toka zizini kwa kutumia gari aina ya Noah. Askari waliokuwa doria walishuku gari hiyo na kuisimamisha, lakini dereva hakusimama na akaongeza mwendo. Askari walilifukuzia na hatimaye, dereva na watu wengine watatu walilitelekeza na kutokomea porini. Jambo la kujifunza ni wezi kwa sasa wamekuwa wakibuni njia mbali mbali ili kufanikisha uhalifu.
Home
Unlabelled
WEZI WAIBA NG'OMBE NA KUMBEBA KWENYE NOAH, MAKAMBAKO - NJOMBE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



Toa Maoni Yako:
0 comments: