Kuwa na NDOTO bila kumiliki hakutoshi kukamilisha NDOTO hiyo. Imani thabiti hutuwezesha kumiliki NDOTO zetu.
Tunamiliki ndoto zetu kwa KUWAZA, KUAMUA na KUTENDA yale yanayotakiwa ili kuitekeleza NDOTO hiyo pamoja na maarifa ya namna ya kuitimiza ndoto hiyo iwe kweli.
Ili kufanikiwa hakikisha UNAIMILIKI ndoto yako kupitia IMANI thabiti UKAWAZE, UKABUNI, UKAAMUE na KUTENDA mambo yanayotafsiri ndoto yako.
Ubarikiwe ewe rafiki yangu mpendwa wa FACEBOOK, USISAHAU kumiliki ndoto yako.
Nakutakia mapumziko mema ya mwisho wa juma.
Cheers.
@ BAGATECH
Godwin D. Msigwa
Dar es salaam
Tanzania
10 Aprili 2016



Toa Maoni Yako:
0 comments: