Mwanzilishi wa taasisi ya Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa akitoa neno la shukrani kwa wageni waalikwa.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benjamin Mkapa Foundation, Dk. Ellen Mkondya Senkoro akitoa historia fupi ya taasisi hiyo kwa wageni waalikwa katika hafla hiyo.

Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya Mkapa Foundation, Balozi Charles Sanga akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kutoa neno katika sherehe za miaka 10 ya taasisi isiyo ya kiserikali ya Mkapa zilioenda sambamba na harambe ya kutunisha mfuko huo.

Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji akizungumza kwenye sherehe za miaka 10 ya Mkapa Foundation zilizoenda sambamba na harambe ya kutunisha mfuko wa taasisi hiyo zilizofanyika April 13, 2016.

Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji (kulia) akijiandaa kukabidhi zawadi ya picha kwa Mwanzilishi wa Taasisi ya Mkapa (Mkapa Foundation), Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa wakati wa sherehe za miaka 10 ya Mkapa Foundation zilizoenda sambamba na harambe ya kutunisha mfuko wa taasisi hiyo zilizofanyika April 13, 2016.

Mgeni rasmi Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha iliyoandaliwa na wafanyakazi pamoja na bodi ya Mkapa Foundation, Mwanzilishi wa taasisi ya Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa wakati wa sherehe za miaka 10 ya taasisi hiyo zilizoambatana na harambee ya kutunisha mfuko wa taasisi hiyo ambapo jumla ya shilingi bilioni moja na milioni mia moja sabini zilichangishwa.

Mgeni rasmi Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji (kushoto) akimkabidhi tuzo Mwanzilishi wa taasisi ya Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa ya kutambua mchango wake wa kuleta matumaini kwa watu wenye mahitaji na kuthamini maono na muongozo kama mwanzilishi wa taasisi ya hiyo iliyoanzishwa mwaka 2006 kwenye sherehe za miaka 10 ya taasisi hiyo iiliyoambatana na hafla ya harambee kwa ajili ya kuchangia taasisi hiyo.

Mgeni rasmi Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji na Mwanzilishi wa taasisi ya Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa kwa pamoja wakizundua jina jipya ambalo ni Mkapa Foundation -"Bringing HOPE to the Underserved".

Picha ya pamoja baada ya uzinduzi.

Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo wabunge na wadau kutoka taasisi na mashirika mbalimbali nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha aliyoinunua kwenye harambee kwa shilingi Milioni 5.5 mgeni rasmi Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji (katikati) ambapo mnada wa picha hiyo uliendeshwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi.

Mwanzilishi wa taasisi ya Mkapa, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa akimpongeza na kumkabidhi Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bank M Tanzania-Plc, Jacqueline Woiso picha iliyokuwa ikipigwa mnada katika sherehe hizo zilizoambatana na harambee ya kutunisha mfuko wa Mkapa Foundation.

Mgeni rasmi Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji akitoa zawadi kwa mwakilishi wa Rais Mstaafu wa Marekani, Bill Clinton.

Picha ya pamoja na wadau wa mashirika mbalimbali, taasisi mbalimbali na sekta binafsi.
---
Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya Benjamini Mkapa jana ilifanikiwa kupata shilingi bilioni moja (1.17 billion) katika hafla ya uchangishaji wa fedha kwa ajili ya kuimarisha sekta ya afya katika maeneo yenye mahitaji maalum nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo muda mfupi baada ya makusanyo hayo, iliyofanyika Dar es Salaam rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa ambaye pia ni muasisi wa taasisi hiyo alisema taasisi binafsi zina mchango mkubwa katika uboreshaji wa afya na uchumi wa nchi.
Mkapa aliwashukuru wadhamini wa hafla hiyo benki ya Bank M na wafadhili wote waliojitokeza ikiwa ni pamoja na makampuni ambao wanaendelea kuiamini na kuifadhili taasisi yake, ili kufikia malengo ya afya bora nchini.
“ Ninaamini sekta binafsi zina mchango mkubwa kwenye uchumi endelevu wa nchi yetu. Hivyo nazishauri sekta binafsi kuwa na ushirikiano wa karibu na serikali pamoja na taasisi za nje kuimarisha huduma za jamii, ikiwemo afya,” alisema.
Kwa upande mwingine aliipongeza serikali ya awamu ya nne chini ya uongozi wa rais mstaafu Jakaya Kikwete, kwa kuisaidia taasisi hiyo kufikia malengo yake, pia anaamini serikali ya awamu ya tano iliyo chini ya John Magufuli itaimarisha zaidi uhusiano.
Naye mgeni rasmi katika hafla hiyo mfanyabiashara maarufu na rais wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited, Mohammed Dewji alisema taasisi hiyo imetoa mchango mkubwa katika kuboresha huduma katika sekta ya afya.
Dewji alisema ili mafanikio hayo yaendelee kuwa bora zaidi, rasilimali fedha na kujitolea inahitajika zaidi.
“Sekta binafsi zina mchango mkubwa wa kusaidia taasisi kama hizi katika kupunguza changamoto zinazoikabili jamii kwa kuwa wafanyabiashara hawawezi kufanya biashara zao katika jamii iliyo na changamoto za afya na uchumi,” alisema mfanyabiashara huyo.
Katika hafla hiyo, Dewji alichangia zaidi ya sh. milioni 200, na kuahidi kuendelea kushirikiana nayo katika kufikia malengo yake.
Awali Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Dk. Ellen Mkondya-Senkoro alisema tangu mwaka 2012 Taasisi ilianzisha utaratibu wa kutafuta rasilimali za kujiendesha hapa hapa nchini kwa kuyashirikisha makampuni, mashirika na taasisi za umma ili kuchangia pia katika miradi mbalimbali ambayo imekuwa inafadhiliwa na wafadhili wa kimataifa.
Tukio hilo lilienda sambamba na maadhimisho ya miaka 10 pamoja na uzinduzi wa jina jipya la ‘Benjamin W. Mkapa Foundation’ na kuondokana na jina la zamani la ‘Benjamin W. Mkapa HIV/AIDS Foundation.

Toa Maoni Yako:
0 comments: