Jamani kuna kundi jipya mjini linafanya mchezo ambao umepata umaarufu kama DOROMESHA! Hii ni operation ya wizi ambayo watu hawa wanakupigia simu na kukueleza kwamba wanahitaji msaada wako.

Number yako ya simu wanakuwa wanaijua na pia watakueleza vitu kadhaa kuhusu wewe ili kuonyesha kwamba wanakujua unafanya kazi gani na mwisho watakuomba mkutane ili mjadili kazi wanayotaka uwafanyie. Mara nyingi huwa tunakua tunafanya dili nyingi za pembeni kuongeza kipato kwahiyo lazima utavutiwa. Mtakutana sehemu tena ya public kabisa na wakati mnafanya mazungumzo, watatoa ofa ya vinywaji au hata chakula. Pale maongezi yatakua ni ya kazi kweli na utajikuta uko serious kujadili kazi na wakati huo huo ndio wanaku DOROMESHA kwa kukuwekea madawa ya kukulewesha ghafla kwenye kinywaji au chakula.

Ukishalewa watakubeba na kuondoka na wewe huku wakiaga kwa kusema kwamba wewe ni rafiki yao na umelewa kwahiyo wanakupeleka nyumbani. Njiani wanakuibia kila kitu mpaka gari na kukutelekeza sehemu uamke baadae.

Ukikutana na watu,

1. Usiagize kinywaji au chakula
2. Usibebe hela au laptop, tablet au vitu vya thamani
3. Hakikisha una mtu au partner wako wa kwenda nae
4. Kuwa makini wakati wote wa mazungumzo na ukihisi unajiskia vibaya, nyanyuka na umuite muhudumu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: