Juma hili kumeibuka kwa kasi kubwa suala la kuwadhalilisha Watanzania kutoka kabila la wasukuma kwa kuwepo kampeni ya kutengeneza picha mbali zinazoonesha watu wakifanya mambo ndivyo sivyo, mfano mtu kunywa tomato source kwa mrija, kufunga seat belt kama kitanzi, kuvua ndala wakati wa kuingia chooni, n,k.
Kwa mtu wa kawaida anaweza kuona ni jambo la kawaida lakini kwangu mimi naona ni mkakati unaolenga kudhalilisha kabila hili kubwa kuliko yote Tanzania na kabila analotoka rais.
Ni mkakati unaofanywa na kundi serious ili kuonesha picha ya wasukuma kuwa hufanya mambo ndivyo sivyo.
Kwa wale ambao wamepasua mbuga za Tanzania watakubaliana na mimi kuwa watu wanaochanganya mambo wapo kila mkoa hapa nchini.
Hili tukilinyamazia litakuwa kubwa na sitashangaa kuona wasukuma nao wakitengeza picha za kuwadhalilisha wachaga kuwa kwenye pesa wapo radhi kutoa mtu roho, watawatengeneza picha za kuonyesha kuwa wanawake wa kihaya wakoje, watatengeneza picha kuonyesha watu wa Mbeya kazi yao ni kulima, watawasema wagogo kuwa wao ni omba omba n.k...
Hii ni kampeni chafu yenye lengo la kuwadhalilisha wasukuma tena purposely kabisa, maana si kabila ambalo ndio lime exist mwaka huu.madhara yake ni makubwa, STOP IT.
( Leonard mapuli)



Toa Maoni Yako:
0 comments: