Naibu waziri wa Fedha na Mipango, Ashatu Kijaji akizumgumza na wahitimu wa chuo cha Mamlaka ya mapato Tanzania TRA leo katika mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere leo jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wahitimu wa chuo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwa katika mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Makamu Mkuu wa Chuo, Lewis Ishemoi akiwaita majina wanafunzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo katika mahafali ya nane ya chuo hicho ikiwa wahitimu 538 wamehitimu mafunzo yao katika chuo hicho jijini Dar es Salaam leo.
Wanafunzi wakivaa kofia zao mara baada ya kutunukiwa katika mahafali yaliyofanika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Wanafunzi wakivaa kofia zao mara baada ya kutunukiwa katika mahafali yaliyofanika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Naibu waziri wa Fedha na Mipamgo, Ashatu Kijaji akiwatunukia vyeti wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao katika mahafali yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Wahadhiri wakiwitunukiwa vyeti pamoja na zawadi mbalimbali katika mahafali ya nane ya chuo cha mamlaka ya mapato (TRA) leo jijini Dar es Salaam. kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Alphayo Kidata na Makamu Mkuu wa Chuo, Lewis Ishemoi.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
---
---
WANAFUNZI
538 wa chuo cha Mamlaka ya Mapato (TRA) wametunukiwa vyeti vyao leo
katika mahafali ya nane ya chuo hicho yaliyofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Pia wahitimu hao wameaswa kuwa waadilifu katika kazi zao kwani taaluma yao ni ukusanyaji wa mapato ya sehemu zao za kazi.
Wameaswa hayo na Naibu
waziri wa Fedha na Mipamgo, Ashatu Kijaji wakati akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa mahafali ya nane
ya chuo cha Mamlaka ya Mapato (TRA) yaliyofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Mwalimu Nyerere.
amesema
kuwa wahitimu wa chuo hicho wafanye kazi kwa weredi na uaminifu kwani
wasipofanya hiyo hawataweza kufanya kazi hayo vile inavyopaswa.
Chuo
cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kitajengwa kingine huko kibaha
mkoani pwani ili kuongeza wanafunzi kusoma katika mazingira mazuri kwani
chuo kilichopo Mwenge kimezungukwa na viwanda.
















Toa Maoni Yako:
0 comments: