Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), Hamis Chagonja
Na Peter Elias, Mwananchi.
Zaidi
ya wanafunzi 52,000 wa mwaka wa kwanza watanufaika na mkopo wa elimu ya
juu baada ya Serikali kuongeza fedha kiasi cha Sh132 bilioni, kwa ajili
ya kugharamia masomo yao kwa mwaka wa masomo wa 2015/16.
Akizungumza
na gazeti hili, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya
Juu (HESLB), Hamis Chagonja alisema bajeti ya Sh341 bilioni ilikuwa
imetengwa kwa ajili ya wanafunzi 14,226 wa mwaka wa kwanza.
Hata hivyo, alisema Serikali imeongeza fedha hizo hadi kufikia Sh473 bilioni ambazo zinatosha kuwalipa wanafunzi 52,000.
Alisema
ongezeko hilo litawawezesha wanafunzi wengine 37,774 ambao hawakuwamo
kwenye bajeti kudhaminiwa na bodi yake kwa mwaka huu wa masomo.
“Kwa
wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao ni 71,125 hatuna shida sana, wao
wataweza kupata fedha hizo. Changamoto ilikuwa kwa hawa wa mwaka wa
kwanza, lakini sasa tumepata fedha za kuwalipa,” alisema.


Toa Maoni Yako:
0 comments: