Kampeni ya First National Bank Tanzania (FNB) kuhamasisha uwekaji akiba miongoni mwa Waanzania imepata mafanikio makubwa kutokana na idadi kubwa ya watumiaji huduma za benki hiyo kuendelea kujitokeza kushiriki.
Mkuu wa kitengo cha bidhaa na huduma za kidigitali wa benki hiyo, Silvest Arumasi, alisema leo kuwa kupitia kampeni hiyo, wateja wapya na wa zamani wanapata nafasi ya moja kwa moja kuingia kwenye droo kutokana na kila elfu hamsini wanayoweka benki.
“Kampeni hii imepata mafanikio makubwa tangu tulipoizindua mwezi Oktoba na inatia moyo kuona idadi ya kuridhisha ya wateja wakishiriki kampeni hii. Zawadi wanazopata washiriki wa kampeni hii zinatokana na viwango vya akiba vinavyowekwa, kwahiyo wateja wanaweza kuongeza uwezekano wa kujishindia zawadi ya shilingi milioni tano kwa kujiwekea akiba zaidi kwenye akaunti zao.”
Kwetu First National Bank, kampeni hii ni njia yetu ya kutoa shukrani kwa wateja wetu kwa kuendelea kutuamini lakini pia wakati huo huo tukiitumia kampeni hii kuielimisha jamii jamii nzima juu ya umuhimu wa kujiwekea akiba,” alisema Arumasi.
“Kwa wale ambao hawajaanza utamaduni wa kujiwekea akiba, kampeni hii inaelimisha juu ya faida za uwekaji akiba na faida zake.”
Arumasi alimtangaza Bw. Boaz Ituwe mfanyabiashara mkazi wa Kimara Dar es salaam kama mshindi wa pili shilingi milioni tano zinazotolewa na benki hiyo kila mwezi kwa mshindi kati ya wateja wanaoshiriki katika kampeni hiyo ya miezi mtatu.
Akiongea baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni tano, mshindi huyo wa aliishukuru benki hiyo na kuwahimiza wananchi kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba.


Toa Maoni Yako:
0 comments: