Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi ameiambia Kajunason Blog kuwa, viongozi wa kisiasa kutoka serikali na upinzani wamekubaliana uchaguzi Mkuu kurudiwa tena.

Hata hivyo, Makamu huyo wa pili amedokeza kuwa hadi sasa haijaafikiwa ikiwa tume ya sasa ya Uchaguzi inayoongozwa na Mwenyekiti Salim Jecha Salim aliyefuta matokeo hayo itakubaliwa kusimamia uchaguzi mpya.

Katika hatua nyingine, kiongozi huyo ameeeleza kuwa rais Ali Mohamed Shein anaendelea kuwa uongozini kikatiba.

Wananchi wa Zanzibar wanasubiri uamuzi wa viongozi wa kisiasa kuhusu mvutano huu wa kisiasa katika visiwa hivyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: