

Moja ya Bango kubwa la "JEMBE" la Mgombea Ubunge wa jimbo la Mafia kwa tiketi ya UKAWA, Ndugu Omary Kimbau maalufu kama JEMBE akiwa pamoja na Madiwani wake katika Kata nane za Jimbo hilo la Mafia katika Wilaya ya Mafia ndani ya Kisiwa cha Mafia.
Na Mwandishi Wetu,
[MAFIA-PWANI] Wananchi wa jimbo la Mafia, jimbo lililopo katika Wilaya ya Mafia ndani ya kisiwa hicho cha Mafia, Mkoa wa Pwani chenye jumla ya Kata Nane, wameombwa kujitokeza kwa wingi Oktoba 25, mwaka huu wampigie kura kwa wingi mgombea wa UKAWA, Omary Ayub Kimbau maalufu kama “JEMBE” ili akawawakilishe Bungeni pamoja na kuwapigania katika kudai haki zao wanamafia.
Hayo yameelezwa kisiwani hapa katika kampeni za mgombea huyo wa Ubunge wa UKAWA, kutokea chama cha Wananchi CUF.
Omary Kimbau ambaye kitaaluma ni msomi wa Biashara na Mwana-Dipromasia, ameweza kufunguka kuwa yeye ni miongoni mwa wanasisa vijana walioweza kupikika kisiasa na kisomi hivyo lengo kuu la kuweza kuwakomboa wananchi wa jimbo hilo ni kumpa nafasi ya kumchagua ili kwenda kuwatetea wananchi wa jimbo hilo pasipokuangalia mtu huyo ametokea familia ya nani ama chama gani kikubwa ni kuakikisha wanampigia kura za wingi za ushindi yeye pamoja na madiwani wote kupitia UKAWA.
“Mimi ni mfanyabiashara na Mwanadipromasia niliyesomea kitaaluma. Nitaendelea kufanya siasa na kusimamia haki kwa wananchi wa jimbo la Mafia na wala si matusi kama wanavyotufanyia wapinzani wetu upande wa pili. Nawaombeni wananchi Oktoba 25, tujitokeze kwa wingi na kukipigia kura CUF kupitia mimi mgobea wenu.. OMARY KIMBAU… pamoja na madiwani wangu wote” alieleza Kimbau katika mkutano huo wa kampeni huku akishangiliwa na umati wa watu wa kijiji hicho cha Banja .
Pia alifunguka kuwa, yeye ndio alikuwa diwani mdogo kuliko wote Tanzania na Duniani aliyewahi kutokea katika ulimwengu wa kisiasa, kwani mwaka 2005, aliweza kuchaguliwa kuwa diwani wa Kata ya Kijitonyama ambapo alikaa kwa kipindi kimoja hadi 2010, ambapo aliacha nafasi hiyo na kwenda kugombea Ubunge ndani ya CCM hata hivyo alinyimwa haki hiyo kwa kuelezwa kuwa yeye ni mdogo licha ya kushinda katika kura za maoni ndani ya chama hicho.
Na kuendelea kusema kuwa, mwaka huu 2015, aligombea tena ndani ya chama cha CCM, katika kura za maoni alifanyiwa zengwe hivyo kukihama chama hicho na kujiunga na CUF ambapo anagombea kwa sasa ndani ya jimbo hilo ambalo amelielezea kuwa anatosha kuvaa viatu vyake.
Hata hivyo aliwataka wanamafia kuachana na kuwapuuza wapinzani wanayoeneza juu ya kumuhusisha na baba yake aliyewahi kuwa kada wa chama hicho cha CCM na mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 20, na kusema kuwa: “CCM wanatapatapa.. na hawana pa kutokea, Hili jimbo ni la “Jembe”. Kule Marekani kulikuwa na Rais George W. Bush ambaye baba aliwahi pia kuliongoza taifa hilo.. tena taifa kubwa Bush alitokea upinzani na wakampa wanachoangalia ni sera na utawafanyia nini.




Kaimu Mwenyekiti wa Wilaya ya Mafia wa CUF, Faki Ally..


Mgombea Udiwani wa Kata ya Kirongwe kwa tiketi ya UKAWA, chama cha CUF, Mohamed Tukhi (kushoto) akifuatilia mkutano huo anayefuatia ni mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CUF, Amdan Rashid Mwinchande.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CUF, Amdan Rashid Mwinchande akitoa sera wakati wa mkutano huo wa kumnadi mgombea wa Ubunge wa UKAWA, Omary Kimbau JEMBE, katika mkutano huo uiofanyika kijiji cha Banja Kata ya Kirongwe.

Amdan Rashid Mwinchande akipeana mkono na Mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo Omaary Kimbau JEMBE..

Wanachama wa CUF wakiserebuka wakati wa mkutano huo..
Faki Ally akimnadi mgombea wa Udiwani wa Kata ya Kirongwe, Mohamed Tukhi..


Mgombea Ubunge wa jimbo la Mafia kwa tiketi ya UKAWA, Omary Kimbau JEMBE , akisalimiana na mgombea Udiwani wa Kata ya Kirongwe, Mohamed Tukhi mara baada ya kumaliza kunadi sera katika Kata hiyo...

Mgombea Ubunge wa jimbo laa Mafia kwa tiketi ya UKAWA, Omary Kimbau akinadiwa na Kaimu Mwenyekiti wa CUF, Faki Ally..

Omary Kimbau JEMBE wa UKAWA/CUF anayegombea Jimbo hilo akijinadi katika mkutano huo wa kampeni katika Kata ya Kirongwe kwenye kijiji cha Banja..

Baadhi ya wananchi wakimsikilia Mgombe wa Ubunge kupitia chama cha wananchi CUF na UKAWA, Omary Kimbau JEMBE, katika mkutano huo wa kampeni katika kijiji cha Banja, Kirongwe.

Baadhi wananchi na wafuasi wa UKAWA wakifuatilia mkutano huo.. wakati Omary Kimbau JEMBE akihutubia jukwaani (Hayupo pichani).

Omary Kimbau JEMBE anayegombea jimbo hilo akitoa fursa za kuulizwa maswali na wananchi wowote wale wa kijiji hicho cha Banja na kujibu ambayo aliielezea ni njia ya demokrasia katika siasa za kisomi na maendeleo..

Omary Kimbau JEMBE anayegombea jimbo hilo la Mafia akiwanadi wagombea wa Udiwani wa Kata nane za jimbo hilo..

Wananchi katika mkutano huo..

Mgombea Udiwani wa Kata ya Kilindoni, Mbonde Mussa akijieleza katika mkutano huo wa kampeni wa kumnadi mgombea Ubunge wa jimbo hilo, Omary Kimbau..

Mgombea Ubunge wa Kata ya Kiegani, Seleman Darushi akijinadi katika mkutano huo..

Mgombea udiwani wa Kata ya Baleni, Omary Baruti akiomba kura..
Kikundi cha hamasa katika mkutno huo cha Rambaramba,wakionesha umahiri wao wa kuimba mashahiri ya papo kwa hapo yanayoendana na kero na matatizo ya jimbo hilo..
Amdan Rashid Mwinchande akiwa katika picha ya pamoja na Mgombea wa Ubunge wa jimbo hilo Omaary Kimbau JEMBE na vijana wa hamasa wa chana hicho.


wananchi katika mkutano huo...







Toa Maoni Yako:
0 comments: