Mandhali ya Jiji la Dar es Salaam yakionekana kuwa shwari kabisaa mara baada ya uchanguzi mkuu ulio fanyika jana
Mtaa wa Samora ukiwa shwari na wananchi wakionekana wakiwa katika shughuli zao za kawaida.
Wananchi wakiendelea na shughuli zao za kawaida
Shughuli za usafiri katika jiji la Dar es salaam zimerudi katika hali ya kawaida baada ya kusimama jana kupisha shughuli za upigaji kura. Hapa ni katika eneo la Stesheni.
Hapa Mnazi Mmoja
Barabara ya Sokoine ikionekana katika hali yake ya kawaida tofauti na jana ambapo ilonekana ikiwa tupu kabisa kotokana na watumiaji wengi wa barabara hiyo kuwa katika pilka pilika za upigaji kura.
Vijana wengi wamerejea katika shughuli zao za kawaida kama wanavyoonekana katika mtaa wa Sokoine tofauti na siku ya jana ambapo mtaa huu haukuonekana kuwa na watu kabisa kutokana na shughuli za upigaji kura.
Katika soko la samaki la kivukoni shughuli zimeendelea kama kawaida baada ya kusimama kwa ajili ya upigaji kura kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika juzi nchini kote.
Barabara ya Uhuru ambayo jana ilikuwa tupu kutokana na wananchi wengi kuwa katika upigaji kura , leo imerejea katika hali yake ya kawaida hasa kwa pilika plika za watu, hapa ni maeneo ya Karume na shughuli zinaendelea kama kawaida.
Hali ilikuwa shwari eneo la Buguruni na wananchi wameendelea na shughuli zao.
Kariakoo nako shwari kabisaa wananchi wanaendelea na shughuli zao
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: