Fuso ikipita Njiani kwenye Maonyesho ya "NDIO Fuso ni Faida" jijini Dar, Maonyesho hayo yanatarijiwa kupita kwenye Mikoa kama Tanga – Moshi- Arusha- Mwanza –Shinyanga -Kahama- Dodoma – Iringa – Mbeya na Songea ambapo shughuli mbali mbali za uchimbaji wa
madini, kilimo, ujenzi na usafirishaji wa mizigo zinafanyika
madini, kilimo, ujenzi na usafirishaji wa mizigo zinafanyika
Wadau wa Usafirashaji wakiwa katika Maonyesho ya 'Fuso ni faida' jijini Dar
Wadau wakipata maelekezo ya Huduma ya 'Ndiyo Fuso ni Faida'
Na Mwandishi Wetu,
Mtandao wa miundombinu ya barabara nchini Tanzania inayokadiriwa kuwa na kilometa za mraba 91,049 ambayo ni mara 30 zaidi ya mtandao wa reli ambayo inaambaa kwenye eneo lenye ukubwa wa takribani kilomita za mraba 3,682 ikidhihirisha kuwa barabara ndiyo njia kuu inayopendelewa kutumika katika usafirishaji wa mizigo.
Usafirishaji nchini Tanzania unajumuisha mitandao ya barabara, anga, reli na maji ambapo katika njia zote hizi, barabara na reli zinaongoza zikifuatiwa na maji na anga. Hakika katika suala la umbali, mtandao wa barabara za Tanzania unashika nafasi ya 51 duniani, kutokana na taarifa zilizonukuliwa katika kitabu “ CIA world fact book”
Wakati ajali za barabarani zikiendelea kugharimu maisha ya watu, ufanisi wa njia hii ya usafirishaji kwa ujumla wake unahitaji kudumisha ubora wa usafirishaji wa barabara nchini Tanzania kutokana na ufanisi wake, kuokoa mda na kuaminika pamoja na kuchukuliwa kuwa kiunganishi kikubwa cha barabara ndogo kwenye barabara kuu za nchi.
Diamond Motors limited hivi karibuni wamekuwa katika safari ya kuzunguka mtandao huu wa barabara wakihamasisha pamoja na mambo mengine usalama barabarani katika kampeni yao ya “Ndio! Fuso ni Faida” Kampeni hiyo iliyozinduliwa mwezi julai mwaka huu jijini Dar es salaam ilifika katika mikoa ya Tanga-Moshi- Arusha – Mwanza – Shinyanga – Kahama – Dodoma – Iringa – Mbeya – na Songea ambapo shughuli mbali mbali za uchimbaji wa madini, kilimo, ujenzi na usafirishaji wa mizigo zinafanyika. Pamoja na mambo mengine, kampeni hiyo ilidhamiria kujenga uelewa kwa wateja wake juu ya jinsi ya kuboresha usafirishaji salama wa mizigo kwa kutumia magari ya kisasa zaidi.
Akifafanua kwa undani juu ya malori mapya yaliyohusika katika kampeni hiyo ya “Ndio! Fuso ni Faida” msemaji rasmi wa kampuni ya Diamond Motors Limited ambao ni wadau na wataalamu katika sekta ya usafirishaji wa masafa marefu kwa kutumia malori yao ya Fuso alisema soko la Tanzania linahakikishiwa malori ya aina ya Fuso FZ na FJ yaliyoboreshwa kiteknolojia na kuwa na uwezo wa kuboresha usalama barabarani. “Malori haya yametengenezwa na kitako imara kilichotengenezwa kwaajili ya uzito mkubwa na mazingira magumu ya kufanya kazi” alisema Meneje Mkuu (Masoko) wa diamond Motors Ltd bwana Laurian Martin. Aliongeza kusema kuwa “tuna nia ya kuborsha sekta ya usafirishaji iliyo bora na salama kwa kutumia malori yetu ya Fuso yaliyo boreshwa ki teknolojia”





Toa Maoni Yako:
0 comments: