Mteja wa bia ya Tusker Bi. Elizabeth Ulomi (katikati) akizungumza na mshereheshaji wa kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habash (kushoto) kabla ya kupokea zawadi yake ya mfuko na fulana wakati wa hafla ya kuipongeza baa ya Coast Pub iliyopo Tangi Bovu-Mbezi beach jijini Dar es salaam ambayo iliibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. Akijiandaa kutoa zawadi hiyo (kulia) ni Msimamizi wa Mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Mbezi beach Obedi Salema. Tofauti na jiji la Dar, kampeni hiyo pia inaendelea mikoa mbalimbali nchini kama Arusha, Moshi, Mwanza, Morogoro na Mbeya.
Bw. Mlai Abraham (katikati) ambaye ni mjasiriamali na mkazi wa Mbezi Beach akizungumza na mshereheshaji wa kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habash (kulia) kabla ya kupokea zawadi yake ya mfuko na fulana wakati wa hafla ya kuipongeza baa ya Coast Pub iliyopo Tangi Bovu-Mbezi beach jijini Dar es salaam ambayo iliibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani. (kushoto) ni Balozi wa bia hiyo Veronica Mbilinyi.
Mpenzi wa bia ya Tusker na mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es salaam, Jane Jeva (katikati) akipokea zawadi yake ya mfuko wenye fulana toka kwa Msimamizi wa Mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Mbezi beach Obedi Salema (Kushoto) katika hafla ya kuipongeza baa ya Coast Pub Tangi Bovu-Mbezi Beach jijini Dar es salaam mara baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker.
Mteja wa muda mrefu wa bia ya Tusker na mkazi wa Goigi, Mbezi Beach aliyefahamika kwa jina moja tu la Chong akiifurahia bia hiyo huku akikabidhiwa zawadi yake ya fulana na Msimamizi wa Mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Mbezi Beach Obedi Salema katika hafla ya kuipongeza baa ya Coast Pub iliyopo Tangi Bovu-Mbezi Beach jijini Dar es salaam mara baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. Promosheni hii inaendelea mikoani pia huku lengo kuu likiwa ni kuhamasisha baa mbalimbali za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli linapokuja suala la utoaji huduma kwa wateja lakini pia kuzisaidia baa hizo kuongeza mauzo ya siku wakati wa promosheni.
Steven Kiswanta ambaye ni mkazi wa Kimara, Dar es salaam akipokea zawadi yake ya fulana na mfuko toka kwa Msimamizi wa Mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Ubungo Victor Mhindi wakati wa hafla ya kuipongeza baa ya Miti Mitatu ya Kimara-Korogwe jijini Dar es salaam ambapo promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ilifunga kambi eneo hilo mwishoni mwa wiki kuipongeza baa hiyo iliyoibuka mshindi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker.


Toa Maoni Yako:
0 comments: