Mpenzi wa bia ya Tusker na raia wa nchi jirani ya Kenya Bw. Oliver
Abanda akipokea zawadi yake ya fulana toka kwa Balozi wa bia hiyo
Veronica Mbilinyi katika hafla ya kuipongeza baa ya Family iliyopo
Tegeta jijini Dar es salaam. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki kwenye
kampeni ya promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na
bia ya Tusker katika kuzihamasiha baa mbalimbali jijini Dar na mikoani
pia kufanya kweli linapokuja swala la utoaji huduma kwa wateja.
Mkazi wa Temeke Maimuna Seif akiifurahia zawadi yake ya fulana toka kwa
Afisa Masoko anayejifunza kwa vitendo toka Kampuni ya bia ya Serengeti
Bw. Josephat Shelukindo katika hafla ya kuipongeza baa ya Kisuma iliyopo
Temeke jijini Dar baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye
promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Kiwanjani inayodhaminiwa na
bia ya Tusker toka Kampuni ya bia ya Serengeti. Promosheni hii ya Tusker
imejikita katika kuziunga mkono baa mbalimbali za mitaa inayotuzunguka
ili kuhakikisha kuwa zinatambulika kwa wateja wa eneo husika na kufanya
kweli kwenye utaoji wa huduma.
Mshereheshaji wa Kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habash
(Kushoto) akizungumza mawili matatu na mteja wa bia ya Tusker na mkazi
wa Tegeta Kibaoni aliyetambulika kwa jina la Libelius Ochungo wakati wa
promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ambayo ilifanyika katika baa
ya Family iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam. Baa hiyo ilitangazwa kama
mshindi wa wiki wa promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker toka
Kampuni ya bia ya Serengeti. Promosheni hii inaendelea pia katika mikoa
ya Arusha, Mbeya, Mwanza, Moshi na Morogoro.
Mpenzi wa bia ya Tusker ambaye pia ni mkazi wa jiji la Mbeya Monalisa
Makangila(Katikati) akipokea zawadi ya fulana na mfuko toka kwa balozi
wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi (Kulia) wakati wa promosheni ya
Tusker Fanyakweli Kiwanjani katika baa ya Kisuma iliyopo Temeke jijini
Dar. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki wa promosheni hiyo inayoendeshwa
na bia ya Tusker toka Kampuni ya bia ya Serengeti. (Kushoto) ni
mshereheshaji wa promosheni hiyo na mtangazaji wa redio Efm Gadner
Habash.
Mfanyabiashara na Mkazi wa Tegeta, Bw. Tungalaza Andrew akipokea zawadi yake ya fulana toka kwa Meneja Masoko wa bia ya Tusker Nandi Mwiyombella wakati wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani wikiendi ya Ijumaa iliyofanyika katika baa ya Family iliyopo Tegeta jijini Dar es salaam. Baa hiyo iliibuka baa ya wiki kwenye promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker toka Kampuni ya bia ya Serengeti.







Toa Maoni Yako:
0 comments: