Kocha wa Timu ya mpira wa miguu ya Sua, Ngabo Jackson (katikati) na
nahodha wa timu hiyo Ally Bakari (kulia wakipokea ngao ya ubingwa wa
Tigo Corporate event kutoka kwa meneja mahusiano John Tungaraza.
Mashabiki wa timu ya Sua wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa kikombe na mbuzi katika bonanza la Tigo Corporate event lililofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Solomon Mahlangu mkoani Morogoro.
Kiongozi wa timu ya kuvuta kamba ya Polisi Morogoro Mwinyi Jumbe, akikabidhiwa zawadi ya mbuzi baada ya kuwa mabinga katika mchezo huo kwaye tamasha la Tigo Corporate Event.
Meneja wa Tigo mkoa wa Morogoro na Tanga, Abasi Abel
akisalimiana na wachezaji wa timu ya polisi chipolopolo katika ufunguzi
wa bonanza la Tigo Corporate Event mkoani Morogoro.
Kijana Alexanda Joeli akikimbia na gunia katika bonaza la Tigo
Corporate Event ilililofanyika katika viwanja vya shule ya msini Solomon Mahlangu, Mazimbu Campus.
Kikundi cha burudani cha Da Hustler dances cha mkoani Morogoro
kikifanya onyesho katika bonanza Tigo Coprorate Event lililofanyika
katika viwanja vya shule ya msingi Solomon Mahlangu Morogoro.
Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya sua Basil Goal Geter akifunga
goli kwa njia ya adhabu ndogo katika mchezo dhidi ya polisi
chipolopolo, katika bonanza hilo timu ya Sua iliibika na ubingwa kwa
kuwafunga Polisi kwa penati 6-5 baada ya dakika tisini kumalizika kwa
sare ya goli moja moja.
Mabigwa wa netball katika bonanza la Tigo Corporate Event timu ya polisi Morogoro wakiongozwa na Angel Anord (katikati) wakikabidhiwa zawadi ya mbuzi baada ya kutwaa ubingwa katika bonanza hilo.


Toa Maoni Yako:
0 comments: