Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Peter Sima na baadhi ya askari wa kikosi hicho wakimsikiliza kwa makini mtaalamu wa kusindika bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emanuel Sawe (kushoto), walipotembea kiwanda hicho, Dar es Salaam kushiriki semina fupi ya wiki ya nenda kwa usalama na TBL.
 Mtaalamu wa kudhibiti Ubora na Ukaguzi wa bia za Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Lydia Raphael (kulia), akifafanua jambo kwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam, Kamishna  Msaidizi Peter Sima, alipotembelea kiwanda hicho  akiwa na baadhi ya Maofisa na Askari kushiriki semina fupi ya wiki ya nenda kwa usalama na TBL.
Wakipata maelezo katika kitengo cha maabara kiwandani hapo
 Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Peter Sima (wa tatu kulia), akishikana mkono na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorice Malulu, baada ya Kamishna huyo na baadhi ya Maofisa na Askari kushiriki semina fupi ya nenda kwa usalama na TBL, Dar es Salaam
Maofisa wa TBL wakiwa katika picha ya pamoja na askari hao Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam,  Kamishna Msaidizi wa Polisi, Peter Sima akiwa katika picha ya pamoja  na baadhi ya Maofisa wa Askari wa kikosi hicho na maofisa wa  Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), baada ya kushiriki semina fupi ya wiki  ya nenda kwa usalama, Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: