Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipata maelezo kuhusu kadi mpya ya Selcom ya kufanyia huduma ya
manunuzi na malipo mbalimbali kutoka kwa Meneja wa Mradi wa Kampuni ya
Selcom Tanzania, Gallus Runyeta, wakati Makamu alipokuwa akitembelea
Mabanda ya maonesho baada ya kufungua Kongamano la Manunuzi ya Umma kwa
Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, lililofunguliwa leo Sept
2, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC Jijini Arusha.
Kadi hiyo inatarajia kuzinduliwa rasmi mwezi Oktoba mwaka huu. Katikati
ni Meneja Mawasiliano wa Selcom, Sabrina Munir.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia wakati akifungua Kongamano la Manunuzi ya Umma kwa Nchi
Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, lililofunguliwa leo Sept 2,
2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC Jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Bilal.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa Kongamano hilo.
Picha za pamoja baada ya ufunguzi wa kongamano hilo.










Toa Maoni Yako:
0 comments: