Mwenyekiti Mweza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari juu ya taarifa iliyeitolewa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam.
Waandishi wakimsikiliza Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA,James Mbatia leo katika hoteli ya New Afrika leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii).
---
Siku moja baada ya Dk Willibrod Slaa kuibuka na kuelezea kilichotokea wakati wa kumkaribisha Edward Lwoassa Ukawa na hatimaye kutangaza kuachana na siasa, Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia amejibu tuhuma zilizotolewa na Dk Slaa huku akitahadharisha kuwa zinalenga kulipasua taifa.
Siku moja baada ya Dk Willibrod Slaa kuibuka na kuelezea kilichotokea wakati wa kumkaribisha Edward Lwoassa Ukawa na hatimaye kutangaza kuachana na siasa, Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia amejibu tuhuma zilizotolewa na Dk Slaa huku akitahadharisha kuwa zinalenga kulipasua taifa.
Mbatia ambaye ni Mwenyekiti Taifa wa NCCR
Mageuzi amesema leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza an
waandishi wa habari kuwa mambo yaliyozungumzwa Dk Slaa ikiwa ni pamoja
na kashfa zakuwatuhumu viongozi wa dini kuhongwa na Lowassa si yakweli
na yanaweza kuligawanya taifa.
Mbatia amesema kuwa Dk Slaa angepaswa kutoa hoja zake na sio kuwashambulia watu binafsi wakiwemo viongozi wa dini.
‘’Mimi
nilitegemea Dk. Slaa ataeleza hoja zake, lakini hoja za kashfa za
kuwahusisha viongozi wa dini hasa maaskofu ni hoja ambazo ni wazi
zimelenga kulipasua taifa’’ alisema Mbatia.
Pia Mbatia
amekiri kuwa Dk. Slaa alishiriki katika mchakato wa kumkaribisha Lowassa
lakini katika vikao vyote Lowassa hakuwahi kusema atakuja na wabunge
toka Chama Cha Mapinduzi.
‘’ Katika kikao cha kujadili
juu ya kumpokea Lowassa tukiwa na viongozi waandamizi wa Ukawa pamoja na
Lowasaa kilichofanyika tarehe 20 mwezi wa saba , Lowassa hajawahi
kutamka kuwa atakuja na wabunge 50 toka Chama cha Mapinduzi, wala
hakusema atakuja na wenyeviti wa mikoa na wilaya’’
Akizungumzia
suala la Dk. Slaa kudai alipewa rushwa ya Sh500m ili kuzuia ripoti ya
Richmond isiingie bungeni, Mbatia ameuliza kwanini Dk.Slaa hakuripoti
kipindi hicho na anakuja kuongelea sasa.
“Nashangaa
tangu sakata la Richmondi litokee ni miaka saba hadi sasa, lakini Dk.
Slaa hakuwahi kusikika akilizungumzia, na kwanini hakuripoti kwenye
vyombo vinavyohusika’’ alihoji Mbatia.
Aidha Mbatia
amevitaka vyombo vya habari kuandaa midahalo maalum ambayo itawahusisha
viongozi wa kisiasi ili kujibu mambo wanayotuhumiwa


Toa Maoni Yako:
0 comments: