Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman Suleiman, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka(wa kwanza kutoka kushoto), leo asubuhi wakati Katibu Mkuu huyo alipotembelea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA) kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria(Terminal 3), leo asubuhi.
 Mkurugenzi wa Mradi wa Jengo la Tatu la Abiria (Terminal III), Mhandisi Mohammed Milanga, akitoa Maelezo ya utekelezaji wa ujenzi wa jengo hilo, kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka wakati alipotembelea eneo hilo leo asubuhi kuona maendeleo ya Ujengo wa jengo la tatu la abiria.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akimsikiliza Mkurugenzi wa Mradi wa Jengo la Tatu la Abiria (Terminal III), Mhandisi Mohammed Milanga, akitoa Maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria hasa eneo la kuingilia abiria wakati alipotembelea eneo hilo leo asubuhi kuona maendeleo ya Ujengo wa jengo la tatu la abiria.Mradi huo kwa sehemu ya kwanza unategemea kukamilika Mwaka 2016.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Dkt Shaaban Mwinjaka( wa tatu kutoka kulia),akiwa katika picha ya Pamoja na Uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania(TAA) pamoja na Mkandarasia anaesimamia ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria mara alipotembelea eneo hilo kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria leo asubuhi.Wa pili kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania(TAA), Mhandisi Suleiman Suleiman.

(Habari Picha na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: