Bw. Moustafa H. Khataw kutoka kampuni ya Skylink akiwakaribisha waandishi wa habari pamoja na wageni waliofika katika droo ya kuwapata washindi wanne leo kwa wateja wote wa Skylink ambao hununua tiketi za usafiri wa ndege kwenda katika nchi mbalimbali duniani.
Mwakilishi wa Shirika la Ndege la Emirates ambao walikuwa ni wadhamini wa shindano Bw.Husain
AlSafi kutoka akiongea
na waandishi wa habari(hawapo pichani) leo katika ofisi za Skylink.
Msimamizi wa bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Bw. Abdallah Hemed akizichanganya vipeperushi ili kuwapata washindi wa droo hiyo
Mwakilishi wa Benki ya Exim akikata utepe wa kuzindua shindano hilo.
Msimamizi wa bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini, Bw. Abdallah Hemed akichanganya karatasi kwa ajili ya kuchagua mshindi.

Waandishi wa habari wakiwa kazini.
Ofisa wa Skylink Solomon Mwale akiwatangaza washindi waliopatikana kwenye droo iliyofanywa na kampuni ya Skylink leo.
Mfanyakazi
wa kampuni ya Skylink wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa
Hyundai ambao walikuwa ni wadhamini mkuu kwenye shindano ilo
---
Hassan Taliki mkazi wa Jijini Dar es Salaam leo ameibuka mshindi na kushinda gari mpya aina Hyundai ix35 katika droo iliyochezeshwa kwenye ofisi za Skylink Jijini Dar es Salaam.
Mshindi huyo amepatikana kutokana na kukata tiketi ya ndege katika Kampuni hiyo hivyo ili aweze kupata zawadi hiyo ametakiwa kwenda na kipeperushi Skylink cha tiketi aliyokana na kitambulisho chake kwa maelekezo zaidi.
Washindi wengine walioshinda kwenye droo hiyo ni Mohamed Swala ambaye ameshinda safari ya kwenda Mahinra kwenda na kurudi huku Issa Nassoro ambaye amekuwa mshindi wa tatu amepata tiketi ya kwenda na kurudi Dubai ambako atapelekwa na Kampuni hiyo .
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ofisa wa Skylink Solomon Mwale alisema kwamba wamepanga kufanya hafla ya kuwakabidhi washindi hao zawadi zao ili umma uweze kuamini kwamba hawabahatishi na droo ikichezeshwa inakuwa ni kweli.
Droo hii ni sehemu ya motisha inayotolewa na Kampuni yetu kwa wateja wote wa Skylink ambao hununua tiketi za usafiri wa ndege kwenda katika nchi mbalimbali duniani.
Droo hiyo imedhaminiwa na Skylink, Hyundai, Emirates, Exim Bank na Club Mahindra.










Toa Maoni Yako:
0 comments: