Mume wa mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha akitoka nje ya Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo.
---
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo imemuachia huru mume wa mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha katika kesi iliyokuwa inamkabili ya kosa la ubakaji baada ya kuona hana hatia juu ya madai hayo.

Mbasha alikuwa anakabiliwa na mashitaka ya kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17.

Muda mfupi baada ya hukumu hiyo kutolewa, Mbasha alipiga magoti mbele za watu na kumshukuru Mungu huku akitokwa na machozi ya furaha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: