Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma(kushoto) akikabidhi jezi kwa kapteni wa timu ya G Unity Fc kwa ajili ya mchezo wa fainali uliofanyika katika kiwanja cha Kipunguni B katika kata ya Kipunguni manispaa ya Ilala jijini Dar. Ambapo timu ya G Unity FC waliibuka washindi baada ya kuichapa timu ya Sukuma Land Fc bao 5 kwa 2.
  Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma(kushoto) akikabidhi jezi kwa kapteni wa timu ya Sukuma Land FC wakati wa mchezo wa fainali wa kombe la Madereva bodaboda wa kata ya Kipunguni.Wa pili kushoto ni ASP Mbunja Matibu kutoka Traffic Makao Makuu.
Maafisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,waratibu wa michezo hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Timu ya Sukuma Land ambapo katika mchezo huo timu hiyo iliibuka mshindi wa pili baada ya kufungwa na timu ya G Unity Fc kwa mambao 5-2.
 
Maafisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF wakiwa kwenye picha ya pamoja na waratibu wa michezo hiyo pamoja na Timu ya G Unity Fc walioibuka washindi wa wa kwanza baada ya kufunga timu ya Sukuma Land Fc mabao 5 -2, mchezo huo uliofanyika katika kiwanja cha Kipunguni B
Mchezaji wa Timu ya Sukuma Land Fc akiwatoka mabeki wa G Unity Fc ambapo katika mchezo huo timu ya G Unity Fc iliibuka mchindi wa mashindano hayo
Ilikuwa ni burudani katika mchezo wa fainali kati ya Timu ya G Unity Fc na Sukuma Land Fc
Gori kipa wa timu ya G Unity FC akijifunga gori wakati wa mchezo wa fainali uliopigwa kwenye uwanhja wa Kipunguni B.
Mkurugenzi mtendaji wa kata ya Kipunguni na Kivule Dr. Kadry Pinde ambaye alikuwa ni Mgeni rasmi katika mchezo wa fainali akikabidhi mpira kwa kapteni wa timu ya Kilimani Fc walioibuka washindi wa wa nne katika mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva Bodaboda wa kata ya Kipunguni. Wa kwanza kushoto ni Afisa Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Ismail Juma.
Mkurugenzi mtendaji wa kata ya Kipunguni na Kivule Dr. Kadry Pinde akiwakabidhi zawadi ya seti ya jezi timu ya Loliondo Fc baada ya kuibuka mshindi wa Tatu katika mashindano hayo.
Washindi wa mashindano ya mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva Bodaboda wa kata ya Kipunguni wakisalimiana mgeni rasimi wakati wa kukabidhiwa zawadi zao
Mkurugenzi mtendaji wa kata ya Kipunguni na Kivule Dr. Kadry Pinde akikabidhi seti ya jezi na mbuzi wawili wa kapteni wa timu ya G Unity Fc ambao waliibuka washindi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa madereva Bodaboda wa kata ya Kipunguni baada ya kuichakaza timu ya Sukuma Land Fc bao 5-2
MAshabiki wakiendelea kufuatia kinachijiri uwanjani
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: