Mchumi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.
Ali Mwatima akifafanua jambo kuhusu masuala ya maafa kwa wananchi
waliotembelea Idara hiyo wakati wa Maadhimisho ya Sherehe za Wakulima
(Nane Nane) tarehe 03 Agosti, 2015 katika viwanja vya Nzuguni Dodoma.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mchumi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu
Bw.Novatus Tesha (wa kwanza kulia) alielezea kitabu cha Taarifa ya
Utekelezaji wa Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne kwa Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Sera na Mipango TAMISEMI Bw. Johnso L. Nyingi
alipotembelea Idara hiyo Agosti 3, 2015 katika maonesho ya Nane Nane
yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni Dodoma. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maonesho ya Sherehe za Wakulima (Nane Nane) yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Toa Maoni Yako:
0 comments: