Meneja Mafunzo ya Biashara wa Airtel Tanzania, Ayubu
Kalufya akitoa elimu kuhusu huduma mpya ya ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’,
wakati wa mafunzo kwa mawakala wa Airtel Money wa mkoa wa Dar es Salaam
jana.
Meneja Mauzo wa Airtel Tanzania Kanda ya Ilala, James Moilo akitoa elimu
kuhusu huduma mpya ya ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’, wakati wa mafunzo kwa
mawakala wa Airtel Money wa mkoa wa Dar es Salaam jana.
Wakala wa Airtel Money Tabata, Sabas Ngwira akiuliza swali kuhusu huduma
mpya ya ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’, wakati wa mafunzo kwa mawakala wa
Airtel Money wa mkoa wa Dar es Salaam jana.
Wakala wa Airtel Money Ukonga, Grace Kimaro akiuliza swali kuhusu
huduma mpya ya ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’, wakati wa mafunzo kwa
mawakala wa Airtel Money wa mkoa wa Dar es Salaam jana.
Sehemu ya Mawakala wa Airtel Money mkoa wa Dar es Salaam wakifuatilia mafunzo kuhusu huduma mpya ya ‘Timiza Mikopo kwa Wakala’, iliyofanyika jijini jana.
---
Kampuni ya Simu za Mkoni ya Airtel imetoa semina kwa Mawakala wa Airtel Money zaidi ya 400 kwa lengo la kuwaongezea mbinu mbalimbali za ujasiriamali huku wakinufaika kupitia huduma ya mikopo kwa wateja maarufu kama Timiza Mkopo kwa Wakala.
Kupitia semina hiyo mawakala wa Kampuni hiyo wataweza kuona fursa mbalimbali za kibiashara na kutumia mikopo hiyo isiyo na dhamana watakayopata kutoka Airtel kukuza biashara zao na kuongeza mitaji.
Akizungumza wakati wa Semina hiyo Meneja Mauzo wa Airtel Money Moses Alphonce alisema kupitia mafunzo hayo mawakala wataweza kuongezea faida zaidi na hatimaye kuboresha upatikanaji wa huduma za kifedha nchini.







Toa Maoni Yako:
0 comments: